Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 3 | USHAHIDI WA AGANO LA KALE KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUTOLEWA KWA AHADI / 153
ya Agano la Kale ambayo ni endelevu na yenye utaratibu mahususi. Je, tufanye nini kuhusu kupuuzwa huku kwa Agano la Kale katika makanisa yetu – je, ni matokeo ya nyakati, au kuna jambo la msingi zaidi nyuma ya hali hii, au sababu ni nyingine kabisa?
Ni Imani Iliyogeuzwa kuwa yaWamataifa? Kama ulikuwa hufahamu, mtazamaji wa kawaida anaweza kuuchukulia Ukristo kama imani yenye mizizi yake katika Utamaduni wa Ulaya, ambayo kimsingi ilianza kama matokeo ya uasi wa Kiprotestanti dhidi ya misimamo mikali ya Kikatoliki wakati wa kipindi cha Matengenezo ya Kanisa katika Karne ya 16 Ulaya. Na si ajabu kwamba mtu angeweza kuwa na mtazamo wa aina hiyo, hasa katika mazingira ya makanisa ya kiinjili, ambayo ni mara chache sana yanarejelea mizizi ya Kiyahudi ya imani ya Kikristo, na hivyo kufanya mada ya chimbuko la Kiyahudi la Imani ya Kikristo kupewa muda mchache au kupuuzwa kabisa katika maisha ya Kikristo yanayoongozwa na maadili na mienendo ya Kimarekani ya tabaka la kati. Kwa bahati mbaya, kuna kuongezeka kwa uadui na chuki katika jamii nyingi za wachache dhidi ya aina za imani ambazo zimevikwa tamaduni za Kikristo, hasa kwa vile wanachukulia neno “Mkristo” kimsingi kama kisawe cha kushikilia kwa kina mitazamo na maadili ya kihafidhina ya wazungu wa tabaka la kati. Kuna ongezeko kubwa la harakati za wanafikra na wasomi ambazo zinarejelea hitaji la kuiondoa imani yetu kutoka katika kongwa na umataifa, wakidai kwamba tumeenda mbali sana katika kutafsiri maisha ya Kikristo kama mfumo wa maadili wa Kiamerika wenye mrengo wa kidini. Kilicho wazi ni kwamba wengi ambao hawavutiwi na mwelekeo huo wa Imani ya Kikristo wanaikataa kabla hata ya kusikiliza kile ambacho Biblia inasema juu ya Yesu wa Nazareti katika Agano la Kale na Agano Jipya. Je, kugundua upya Agano la Kale (kwa lugha rahisi, kitabu cha kipekee cha Kiebrania) kunawezaje kutusaidia kufikia ukomavu wa kina zaidi ya mwelekeo wa kuifanya sehemu kubwa ya imani na maisha ya Kikristo leo kuwa ya utamaduni wa wamataifa? Ngumu Sana na Isiyoelewa Hivi majuzi, kiongozi wa kikundi cha vijana msomi na anayependwa katika kanisa fulani linalokua alishangazwa kuona kwamba ni washirika wachache tu wa kikundi chake cha vijana walioonyesha kuwa na uelewa angalau wa hadithi na watu muhimu wa Agano la Kale. Na hapa hatuzungumzii baadhi ya wahusika wadogo wa AK, la hasha! Tunaongelea watu kama Musa, Eliya, Elisha, nk. Katika kujaribu kurekebisha ugumu huu, kiongozi huyo wa kikundi cha vijana alianzisha mfululizo wa mafundisho ya Biblia yenye kichwa “Nyakati Muhimu” ambao ulikusudiwa kuangazia mambo
3
3
M A S O M O Y A B I B L I A
4
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker