Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
154 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
muhimu yaliyochaguliwa ya Agano la Kale na kuonyesha jinsi yanavyohusiana na Kristo na Ufalme wake unaozungumzwa katika Agano Jipya. Baada ya wiki chache, mwenendo wa kikundi cha vijana ilibadilika sana. Baadhi ya wanafunzi, wakidai kuwa hadithi na maudhui hayo ya AK kuwa magumu sana na yasiyosisimua kabisa, waliacha kuhudhuria katika kikundi kabisa. Wakati huo, kikundi kingine kiliona hadithi hizo kuwa za kustaajabisha, lakini hazihusiani kwa namna yoyote na mahali wanapojiona kimaisha. Kikundi kingine kidogo, hata hivyo, kimestawi chini ya mafundisho hayo, na kwa mara ya kwanza wanaamini kwamba wamepata fursa ya kulielewa Agano la Kale. Shinikizo linaongezeka katika kanisa kwamba watu warudi kwenye mfumo wa mafundisho wa siku za zamani ambapo walifundishwa juu ya masuala ya kisasa ambayo yalikuwa rahisi kufundisha (na kusikiliza!), lakini kiongozi amedhamiria kumaliza mfululizo huo wa AK, ambao unahitaji miezi mitatu zaidi kuukamilisha. Ikiwa kiongozi wa kikundi cha vijana angeuliza maoni yako, ungemshauri vipi juu ya kulifanya Agano la Kale kuwa hai na la kusisimua katika kikundi chake bila kuwatenga na kuwachanganya baadhi ya “ndugu dhaifu” wanaolalamikia mafundisho yake? Uhusiano wa Agano la Kale na Agano Jipya unaweza kueleweka vyema kupitia wazo la ufunuo endelevu , ambao unathibitisha kwamba Mungu amejifunua hatua kwa hatua na kwa uhakika katika historia ya watu wake, na hatimaye kupitia Yesu Kristo. Mungu kwa namna mbalimbali na nyakati tofauti-tofauti alijidhihirisha kwa taifa la Israeli kwa kiwango fulani, lakini katika siku hizi za mwisho amesema nasi wazi wazi kwa njia ya Mwanaye. Yesu wa Nazareti ndiye ufunuo wa mwisho na kamili wa Mungu juu yake mwenyewe, ambao sasa unashuhudiwa katika Maandiko. Kama asemavyo Agustino: “Katika Agano la Kale Agano Jipya limefichwa; katika Agano Jipya Agano la Kale limefunuliwa.” Uhusiano wa AK na AJ uhusiano kamilishi, Agano la Kale likitoa utangulizi wa hitimisho la Agano Jipya kuhusu Kristo, Agano la Kale linasimama kama matarajio ya kilele cha Agano Jipya kuhusu hadithi ya wokovu wa Mungu katika Kristo. Zaidi ya hayo, Agano la Kale linaonyesha utu wa Kristo na kazi yake iliyojumuishwa kikamilifu katika Agano Jipya. Ingawa Agano la Kale ni ufunuo wa awali na hafifu wa wokovu wa Mungu, Agano Jipya linaweza kuonekana kama la mwisho lililokamilishwa, na wito wa ulimwengu wote ambao katika Agano la Kale umeainishwa kimahususi kwa taifa la Israeli. Muunganiko wa maagano haya unaweza kuonekana katika ahadi na mada ya utimilifu, hasa kwa namna Agano Jipya linavyothibitisha kwamba kazi ya Agano la Kale ni kutoa ushuhuda wenye nguvu na wa uhakika kuhusu Masihi, kupitia historia ya mababa wa imani, Taifa la Israeli, unabii mbalimbali juu ya Masihi, na viwango vya maadili vya Sheria.
Marudio ya Tasnifu ya Somo
3
M A S O M O Y A B I B L I A
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker