Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | USHAHIDI WA AGANO LA KALE KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUTOLEWA KWA AHADI / 155

Mada kuu inayounganisha ufunuo wote wa Biblia katika Maandiko ni mada ya ahadi na utimilifu . Mada hii inathibitisha umoja wa Agano la Kale na Agano Jipya, katika suala la dhamira ya Mungu kujidhihirisha mwenyewe, kuwakomboa watu wake, na kufanya hivyo kupitia ahadi iliyotolewa kwa Ibrahimu na uzao wake ambayo ilitimizwa katika Yesu wa Nazareti. Andiko kiini linaloelezea ahadi hiyo ni protoevangelium , tamko la kwanza la Injili katika Mwanzo 3:15. Hapa Mungu anaahidi uhakika wa uadui kati ya nyoka na mwanamke na “uzao” wao husika, kupondwa kwa kisigino cha mzao wa mwanamke, na kupondwa kichwa cha nyoka na mzao huyo wa mwanamke. Katika Agano Jipya, Yesu wa Nazareti anafunuliwa kuwa uzao huu wa kiungu aliyetumwa kuharibu kazi ya ibilisi na kuwakomboa wanadamu kwa ajili ya Mungu. Ahadi ya Yehova ya agano na Ibrahimu inatumika kama mwendelezo wa hatua kwa hatua wa ahadi takatifu ya Mungu ya kumleta Mwokozi. Katika agano lake na Abrahamu, Mungu aliahidi kumpa “uzao” ambao ungeleta ukombozi na urejesho kwa wazao wa Abrahamu na mataifa yote ya dunia. Katika Agano Jipya, Yesu wa Nazareti anatangazwa kuwa uzao wa Ibrahimu, mrejeshaji na mkombozi wa uumbaji na ulimwengu. Kama unapenda kujifunza kwa kina baadhi ya mawazo yaliyomo katika somo hili la Kutolewa kwa Ahadi , jaribu kusoma vitabu vifuatavyo: Baron, David. Rays of Messiah’s Glory: Christ in the Old Testament . Eugene, OR: Wipf and Stock Publishers, 2001. Clowney, Edmund P. The Unfolding Mystery: Discovering Christ in the Old Testament . Phillipsburg, NJ: P & R Publishing, 1991. Drew, Charles D. The Ancient Love Song: Finding Christ in the Old Testament . Phillipsburg, NJ: P & R Publishing, 2000. Unapopitia somo hili, ukichunguza asili ya ushuhuda wa Agano la Kale kwa habari ya Kristo, utahitaji kuchunguza njia ambazo maarifa na mitazamo hii inaweza kuathiri uelewa wako mwenyewe na utendaji wako katika huduma. Je, unasomaje na kuchunguza Agano la Kale, una mitazamo na mwitikio wa namna gani kuhusu fasihi ya Agano la Kale, na ni kwa njia gani mahubiri na mafundisho yako yanahitaji kuathiriwa na uelewa mpya na wenye umoja zaidi wa uhusiano wa maagano haya mawili? Mwombe Roho Mtakatifu akusaidie kutambua njia kuu ambazo unaweza kuhitaji kuhusianisha moja kwa moja huduma yako kwa vitendo na mitazamo na mawazo ambayo umejifunza katika somo hili, na yale ambayo unaweza kufikiria na kuombea katika wiki hii yote ijayo. Ufunguo wa ukuaji wa nguvu na uvumbuzi katika huduma ni kuwa wazi na tayari

Nyenzo na Bibliografia

3

M A S O M O Y A B I B L I A

Kuhusianisha Somo na Huduma Ukurasa wa 89  9

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker