Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

156 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

kwa maongozi ya Roho Mtakatifu kuhusu ukuaji, mabadiliko, na matumizi ya maarifa ya kimungu. Mwombe akuonyeshe hali yoyote ambapo unaweza kutumia maarifa haya mapya katika maisha yako binafsi na huduma.

Tumia muda katika maombi kwa ajili yako na wenzako, ukimwomba Mungu kwamba akuwezeshe kukua katika ujuzi na matumizi yako ya dhana za kibiblia za ufunuo endelevu, ahadi na utimilifu, na ustadi na uthamini wako wa umoja uliopo katika Agano la Kale na Agano Jipya. Mwombe Mungu akupe upendo na utambuzi mpya wa ufunuo wa Biblia kuhusu ukuu wa Yesu Kristo, na umwombe ujazo mpya wa Roho Mtakatifu ili uweze kuthibitisha kwa uzoefu msemo wa Agustino: “Katika Agano la Kale Agano Jipya limefichwa; katika Agano Jipya Agano la Kale limefunuliwa.” Maombi ni njia yenye nguvu, yenye matokeo, na iliyoamriwa na Mungu ya kupokea hekima yake (Yakobo 1:5), usidharau kamwe nguvu ya maombi katika kujifunza kwako Neno la Mungu. Jiombee kwa bidii wewe mwenyewe na wanafunzi wenzako, na umwombe Bwana upaji na usaidizi wake uliojaa ukarimu – yuko tayari zaidi kuutoa.

Ushauri na Maombi Ukurasa wa 90  10

KAZI

3

Luka 24:44-48

Kukariri Maandiko

M A S O M O Y A B I B L I A

Ili kujiandaa kwa ajili ya darasa, tafadhali tembelea www.tumi.org/ books ili kupata kazi ya kusoma ya wiki ijayo, au muulize Mkufunzi wako.

Kazi za Usomaji

Kama kawaida unapaswa kuja na Fomu ya Ripoti ya Usomaji yenye muhtasari wako wa kazi ulizopewa kusoma kwa wiki. Pia, ni muhimu uwe umechagua maandiko utakayotumia katika kazi yako ya ufafanuzi wa Maandiko (eksejesia) na utoe mapendekezo yako kuhusiana na kazi ya huduma kwa vitendo.

Kazi Zingine Ukurasa wa 92  11

Katika somo letu linalofuata, Ushahidi wa Agano Jipya kuhusu Kristo na Ufalme Wake: Kupingwa kwa Masihi , tutachunguza dhana ya Kiyahudi ya Ufalme wa Mungu wakati wa Yesu. Tutaona jinsi taifa la Israeli, lililokandamizwa na dola za kisiasa, liliamini kwamba Masihi atakapokuja, Ufalme wa Mungu ungekuja kwa nguvu, kuleta urejesho wa ulimwengu unaoonekana na kuokoa wanadamu kutoka katika udhibiti wa Shetani. Bila shaka, Yesu aliutangaza Ufalme kama

Kuelekea Somo Linalofuata

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker