Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

164 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

C. Mtazamo wa ulimwengu wa Kiyahudi kuhusu Ufalme wakati wa Yesu Ufuatao ni muhtasari wa mawazo machache ya msingi yaliyoshikiliwa na waumini wa Kiyahudi ambao walikuwepo wakati wa Yesu alipokuja mara ya kwanza. Mawazo haya yanachukuliwa kuwa yalitumika kama msingi wa matukio na mafundisho ya Maandiko ya Kiebrania (yaani, Agano letu la Kale).

1. Mungu ndiye Mfalme wa mbingu na dunia yote (kama Muumba wa ulimwengu wote, yeye peke yake ndiye aliye na haki kamili ya kutawala vitu vyote vizuri alivyoumba).

2. Haki kuu ya Mungu ya kutawala imepingwa katika ulimwengu mzima.

a. Imepingwa na “ Shetani ” (= “adui”), kiumbe wa kiroho ambaye aliasi haki ya Mungu ya kutawala.

b. Kupitia udanganyifu wa Shetani, wanadamu walianguka katika uasi, wakapoteza uhuru wao chini ya Mungu, na kuingia chini ya udhibiti wa mamlaka na utawala wa Shetani.

4

M A S O M O Y A B I B L I A

c. Kwa sababu ya uasi wao dhidi ya Mungu, wanadamu wamehama kutoka katika Ufalme wa Mungu (utawala na ushawishi wa Mungu) hadi ufalme wa Shetani (utawala na ushawishi wa shetani).

3. Ufalme wa shetani unatawala katika mfumo wa ulimwengu wa sasa.

a. Ushawishi wake na uwepo wake unagusa awamu zote za utaratibu huu wa ulimwengu wa sasa.

b. Ufalme wa Shetani unafanya kazi katika ulimwengu wa kimwili na katika mambo ya wanadamu.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker