Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 4 | USHAHIDI WA AGANO J IPYA KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUPINGWA KWA MASIHI / 165

4. Falme hizi mbili, yaani Ufalme wa shetani na Ufalme wa Mungu , ziko katika vita na mapambano makuu.

a. Mungu anathibitisha tena haki yake ya kutawala uumbaji wake, na ufalme wa shetani unapinga juhudi hii kwa ghadhabu na nguvu zake zote.

b. Suala katika vita hivi ni hili: nani atakuwa na haki kamili ya kutawala na kumiliki juu ya uumbaji na wanadamu .

D. Maono maalum ya Israeli ya Ufalme kuhusiana na utambulisho wake. Wazo la Ufalme liliathiri namna Wayahudi walivyotafsiri upinzani wa kiroho na uhusiano wake na nguvu za ulimwengu wa kimwili, mambo ya kibinadamu, na mahali pa Israeli kama taifa.

1. Israeli kama taifa limeingizwa katika pambano hili kati ya Mungu na Shetani kwa ajili ya kuitawala dunia.

4

a. Wao ni watu maalum wa Mungu kwa sababu ya Agano, Mwa. 12-17.

M A S O M O Y A B I B L I A

b. Ingawa wameitwa kuwa watu maalum wa Mungu, wanaishi katika mazingira (hali) ambayo yanatawaliwa na ufalme wa Shetani . (1) Nguvu za kisiasa, za kiserikali, na za kijamii ambazo zilikuwa na uadui dhidi ya Israeli kwa kweli ziko chini ya udhibiti wa Shetani. (2) Mungu alitumia mifumo hii kwa makusudi yake (ingawa hawalikujua hilo).

2. Ufalme wa Mungu ungekuja kwa nguvu kupitia Masihi na ungekomesha udhibiti na uvutano wa Shetani juu ya ulimwengu na wanadamu.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker