Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

166 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

a. Uvamizi wa ajabu wa nguvu za Mungu ili kukomesha mara moja na kwa wakati wote udhibiti wa Shetani juu ya wanadamu. (1) Uvamizi wa ufalme wa Mungu ungekuwa mara moja (ungetokea ghafla). (2) Uvamizi wa ufalme wa Mungu ungeleta mapinduzi makuu (ungehusisha ulimwengu wote). (3) Uvamizi wa ufalme wa Mungu ungekuwa wa kukata shauri (ungekomesha utawala wa Shetani).

b. Badiliko la uteka kwa watu wa Mungu (yaani, kupitia ujio wa Ufalme, Israeli ingekuwa taifa kubwa zaidi kuliko mataifa yote duniani).

3. Ufalme wa Mungu ungekuja kupitia ukoo wa wafalme wa Kiebrania.

a. Wafalme wa Waebrania walikuwa watawala chini ya mamlaka ya Mungu.

b. Ufalme wa Mungu ungekuja kupitia ukoo wa wafalme wa kizazi cha Daudi (2 Sam. 7; Zab. 89).

4

M A S O M O Y A B I B L I A

c. Masihi anatamkwa mara nyingi katika Maandiko ya Agano la Kale kama “ mwana wa Daudi ” (taz. Isa. 9:6 7; Yer. 23:5-6; Zab. 2).

d. Kutokea kwa Masihi kungekuwa uthibitisho kwamba Siku ya Bwana imefika, na kwamba Ufalme umekuja.

4. Ujio wa Ufalme wa Mungu ungeleta mabadiliko makubwa.

a. Ungetokeza ukombozi wa taifa la Israeli kutoka katika ukandamizaji wa kisiasa na kutawaliwa .

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker