Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 4 | USHAHIDI WA AGANO J IPYA KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUPINGWA KWA MASIHI / 167

b. Ungesababisha kuburudishwa na kufanywa upya kwa uumbaji wote kurudi kwenye utukufu na fahari yake kama Edeni .

c. Ungeleta amani na uadilifu katika haki kati ya mataifa yote, Israeli ikiwa kichwa chao.

d. Ungetokeza mabadiliko ya kiroho ya kimataifa , huku mataifa yote yakibadilika na kumtumikia na kumwabudu Mungu wa kweli, YHWH.

e. Ungekuwa wa kimafunuo katika uwezo wake: ungetokea ghafla, katika siku zijazo, na kuathiri ulimwengu wote, wa kimwili na mambo ya kibinadamu.

II. Kuja kwa Yesu Ni Uwepo wa Ufalme wa Mungu Hapa na Sasa: Anapinga na Kushinda Athari za Laana na Ufalme wa Ibilisi.

A. Yesu Kristo katika nafsi yake anawakilisha Ufalme wa Mungu hapa na sasa .

4

1. Yesu alijitangaza kuwa Masihi aliyeahidiwa ambaye kupitia yeye madhara yote ya laana, dhambi, ukandamizaji wa kishetani, na ukosefu wa haki za kijamii yangekomeshwa.

M A S O M O Y A B I B L I A

a. Kwa kuja kwake, alitangaza kwa kuja kwa Ufalme “sasa”, Mk 1:14-15.

b. Alijitangaza kuwa Mtumishi wa Yehova ambaye angekomesha udhalimu wote, Luka 4:18-19.

c. Yeye ni Neno aliyefanyika mwili , udhihirisho halisi wa Mungu katika umbo la mwanadamu alikuja duniani (Yohana 1:14-18).

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker