Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 4 | USHAHIDI WA AGANO J IPYA KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUPINGWA KWA MASIHI / 169

6. Kazi ya Masihi Yesu ya kufukuza mapepo inawakilisha “kufungwa kwa mtu mwenye nguvu” kama ilivyonenwa katika Luka 11:14-20.

7. Tabia isiyo na kifani ya Masihi inadhihirisha utukufu na ukuu wa Baba mwenyewe, Yoh. 1:14-18.

8. Kifo cha Masihi kinawakilisha malipo ya deni letu la dhambi na adhabu yake, pamoja na kushindwa kwa Shetani, kama Paulo asemavyo katika Wakolosai 2:15, Kristo alifanya onyesho la wazi la ushindi wake msalabani, ambapo deni la dhambi na udhalimu wetu lililipwa kikamilifu.

C. Ufalme Upo Tayari, Lakini Bado: aina mbili za madhihirisho ya Ufalme wa Mungu.

1. Kupitia uwepo wa Yesu, Ufalme ulidhihirishwa, na utawala wa Mungu ukaanzishwa. Kupitia kifo na ufufuo wake, yule mkuu mwasi, Shetani, mdanganyifu mkuu na mkufuru alijeruhiwa, alitiwa kilema, amefungwa, lakini uharibifu wake unakuja baadaye, taz. 1 Yoh. 3:8; Ebr. 2:14-15; Kol. 2:15. 2. Katika Ujio wa Pili wa Kristo (kile ambacho wasomi hukiita Parousia [Kiyunani cha “Kuwasili kwa Mara ya Pili”]) Shetani ataangamizwa hatimaye, utawala wake hatimaye utaangushwa, na udhihirisho kamili wa uwezo wa kifalme wa Mungu utafunuliwa kupitia kutukuzwa kwa watakatifu, na kuletwa kwa mbingu mpya na nchi mpya, 1 Kor. 15:24-28.

4

M A S O M O Y A B I B L I A

III. Masihi Akabiliana na Upinzani wa Nguvu za Giza: Kazi za Uponyaji na Kutoa Pepo katika Maisha ya Yesu

A. Ufalme umekuja katika Yesu: uponyaji na miujiza

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker