Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
172 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
Conclusion • Yesu ndiye utimilifu wa ahadi ya Kimasihi ya Agano la Kale katika tumaini lake la kuja kwa Ufalme. • Kuja kwa Masihi katika Yesu kulitofautiana na mtazamo wa Kiyahudi wa wakati ule, na bado kulitimiza ahadi za Kimasihi za Ufalme. • Yesu kama Masihi alipata upinzani kutoka nguvu kubwa za giza na alizishinda wakati wa huduma yake ya hadhara duniani, ikijumuisha madhara ya laana na ubwana ulioasi wa shetani. Maswali yafuatayo yalikusudiwa kukusaidia kupitia maudhui yaliyomo katika video. Katika utu wa Yesu wa Nazareti Ufalme wa Mungu umekuja, ukithibitisha tena haki ya Mungu ya kutawala katikati ya ulimwengu unaosumbuliwa na matokeo ya laana na uonevu mbaya wa shetani. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko! 1. Katika aya fupi au maelezo machache, eleza vipengele mbalimbali vilivyounda dhana ya Kiyahudi ya Ufalme wa Mungu wakati wa Yesu. Kwa nini Wayahudi wa siku za Yesu waliona ni vigumu kuamini kwamba yeye, mwana wa seremala mnyenyekevu kutoka Nazareti, huenda kweli akawa ndiye Masihi? 2. Kuhusiana na kipengele cha wakati, wazo la Kiyahudi la Ufalme lilitofautianaje na maoni ya Yesu mwenyewe kuhusu kuja kwa Ufalme? 3. Ni katika maani ipi Yesu anatangaza kwamba unabii wa Ufalme wa Mungu unaokuja umetimizwa katika yeye wakati wa huduma yake? Kuwa mahususi katika jibu lako. 4. Uponyaji wa Kristo na kufukuza mapepo unadhihirishaje kwamba ahadi ya Ufalme wa Mungu imetimia kweli kweli katika siku za Yesu mwenyewe? 5. Kukabiliana kwa Yesu na nguvu za adui kunaonyesha mamlaka yake katika ulimwengu huu. Mgogoro huo unatusaidiaje kuelewa huduma ya Masihi ulimwenguni leo? 6. Ikiwa Ufalme umekuja ndani ya Yesu, basi kwa nini nguvu zote za uovu na ushawishi wake hazijaharibiwa kabisa? Je, kuna mwelekeo wa wakati ujao ambapo Yesu ataukamilisha uwepo wa Ufalme, na ikiwa ndivyo, ni nini?
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
4
M A S O M O Y A B I B L I A
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker