Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 4 | USHAHIDI WA AGANO J IPYA KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUPINGWA KWA MASIHI / 173
7. Yesu wa Nazareti anatimiza ahadi ya ufalme, na kwa hiyo kama Masihi anakabiliana na madhara ya laana na kazi za ufalme wa giza. Je, tunatumiaje mamlaka haya ya ufalme katika huduma na maisha yetu wenyewe, hapa katikati ya jiji?
UHUSIANISHAJI
Somo hili linaangazia upinzani alioupata Bwana wetu, si tu kutoka kwa watu wa wakati wake katika taifa la Israeli, bali zile nguvu kubwa zaidi za kiroho za laana, shetani, na uovu wa kimaadili unaofanya kazi duniani. Yesu wa Nazareti anatimiza ahadi ya ufalme wa Mungu, akisimika tena utawala wa Mungu duniani, na kuonyesha dhahiri kupitia maisha yake na kazi yake ushindi wa Mungu juu ya dhambi, Shetani, na kifo. • Dhana ya Kiyahudi ya Ufalme wa Mungu wakati wa Yesu, iliyochochewa na ukandamizaji waliokuwa wakiupitia kutoka kwa mamlaka za dola zilizotawala, na ilihusisha pia imani yao kwamba Ufalme wa Mungu utakuja kwa nguvu, kurejesha ulimwengu unaoonekana na kuokoa wanadamu kutoka katika udhibiti wa Shetani. • Maoni ya Yesu kuhusu Ufalme yalipingana na watu wa siku zake kwa sababu Yesu alitangaza Ufalme kuwa ndani yake mwenyewe na kazi zake za nguvu, jambo lililodhihirishwa katika uponyaji wake na kutoa pepo. • Akiwa ndiye Masihi wa kweli ingawa asiyetarajiwa, Yesu alizikabili zile nguvu za kiroho ambazo zimeshikilia ulimwengu na jamii ya wanadamu mateka tangu anguko. • Yesu wa Nazareti anatimiza ahadi ya Ufalme, na kwa hiyo kama Masihi anayakabili madhara ya laana na kazi za ufalme wa giza. Sasa ndio wakati wa wewe kujadili pamoja na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu maana halisi ya upinzani wa Yesu katika maisha na huduma yake akiwa Masihi katika Israeli. Muhtasari mfupi wa fundisho la kibiblia la upinzani wa Yesu unaonyesha kwamba kanuni ya msingi ya kazi ya Yesu ilikuwa kupitia mzozo usiokoma na wale waliompinga katika kazi yake ya kuendeleza ufalme. Unapofikiria kipengele hiki muhimu cha kazi ya Masihi, ni aina gani ya maswali uliyo nayo kuhusu maisha na huduma yako mwenyewe? Je, upinzani na migogoro inaathiri vipi viwango mbalimbali vya huduma yako kwa Bwana leo? Labda baadhi ya maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kukusaidia kutengeneza maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi.
Muhtasari wa Dhana Muhimu
4
M A S O M O Y A B I B L I A
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker