Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

174 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

• Je, kiwango na kujirudia tena na tena kwa upinzani, migogoro, na mateso katika maisha ya Yesu kinatuambia nini kuhusu hali ya huduma zote za kuendeleza Ufalme leo? • Ni kwa kadiri gani mwanafunzi wa Yesu leo anaweza kutazamia kukataliwa na upinzani ulioambatana na maisha ya Yesu? Ni katika njia zipi maisha ya Yesu ni kielelezo kwetu, na ni kwa njia gani maisha yake ni ya kipekee kabisa na mahususi kwake peke yake? Elezea. • Yesu wa Nazareti anatimiza ahadi ya ufalme ndani yake, kwa hiyo, kwa maana halisi, Ufalme wa Mungu umekuja. Aina hii ya mafundisho ina maana gani kwa huduma na maisha katika maeneo ya mijijini? Je, kuna dalili za Ufalme kuja katika eneo la ujirani wako? Wapi? • Namna gani aina ya injili inayoahidi utajiri na afya inapatana au kupingana na maoni ya Yesu kuhusu Ufalme kuja kupitia nafsi yake mwenyewe? • Kwa maana fulani, Ufalme wa Mungu tayari uko hapa, lakini bado haujakamilishwa (yaani, Ufalme ambao ni Tayari/Bado). Ni vipengele vipi vya Ufalme wa Mungu ambavyo bado vinangoja ukamilisho na udhihirisho kamili katika Ujio wa Pili wa Yesu? • Ni kwa njia gani huduma za Kanisa zinaendelea kuonyesha namna Yesu wa Nazareti anavyotimiza ahadi ya ufalme kupitia ushindi wake juu ya madhara ya laana na kazi za ufalme wa giza? Ukandamizwaji wa Kipepo, Kumilikiwa, au Vyote viwili? Ukweli kwamba Ufalme wa Mungu umekuja katika nafsi ya Yesu unafafanua kabisa uhusiano wa mwamini na wa Kanisa na shetani. Kwa sababu ya kazi ya Yesu msalabani, mwamini hayuko chini ya utawala na nguvu za shetani tena; ushindi wa Mungu unapatikana kwa kila mwamini anayekiri kwamba kazi ya Kristo ni yake (1 Yoh. 3:8; Ebr. 2:13ff; Yak. 4:7; 1 Yoh. 5:4; Efe. 6:10-18; 2 Kor. 10:3-5). Je, kuna uwezekano gani wa waumini kukandamizwa na mapepo, kuingiwa na mapepo, au vyote viwili, au haupo kabisa? Muumini anapaswa kufanya nini ili kupata ushindi endelevu unaopatikana kwake kupitia dhabihu ya damu ya Yesu (Ufu. 12:9-)?

4

M A S O M O Y A B I B L I A

MIFANOHALISI

1 Ukurasa wa 100  6

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker