Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 4 | USHAHIDI WA AGANO J IPYA KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUPINGWA KWA MASIHI / 175
Je, Mateso ni Lazima kwa Mwamini? Kwa mujibu wa Paulo, waaminio wamepewa si tu kumshikilia Bwana Yesu kwa ujasiri, bali pia kuteseka kwa ajili yake (Flp. 1:29-). Wapo wengine wanaofundisha Injili kana kwamba ushindi alioupata Bwana wetu juu ya dhambi na shetani unamaanisha kivitendo kwamba hatuwezi tena kupitia nyakati za mateso na dhiki. Mafundisho haya yanajaribu kusadikisha watu kwamba mwamini anapofikwa na magonjwa, huzuni, kuhangaika, mashaka, au maumivu, basi lazima shida iwe ni kwake mwenyewe, kwa sababu ya ukosefu wa imani. Je, unaweza kuelezeaje ulazima wa kuteseka au kutolazimika kuteseka katika maisha ya mfuasi mcha Mungu wa Yesu Kristo? Je, ni lazima kila mwamini aliyeoshwa kwa damu pia atazamie ubatizo wa moto wa mateso kutoka kwa adui na maadui wa Mungu, au je, yanaweza kuepukwa kabisa kwa kutembea kikamilifu pamoja na Mungu? Je, ni Aibu kwa Kristo? Fundisho la kawaida katika duru nyingi za kiinjili ni kwamba Bwana wetu alikufa waziwazi ili kuondoa uwezekano wa kuwepo kwa mambo fulani mabaya ambayo tungeweza kukumbana nayo na kuyapitia. Wanakiri kwa kupigwa kwake sisi tumepona, na hii ina maana kwamba tunapaswa kuendelea kukiri afya isiyokoma na ustawi endelevu kwa msingi wa mateso ya Yesu msalabani. Ukweli kwamba Kristo aliteseka kwa ajili ya mambo haya ina maana kwamba mwamini hapaswi kujaribu kumwaibisha Kristo kwa kupuuza ushindi wake au kuupunguza uzito kwa sababu ya imani dhaifu au isiyo ya kibiblia. Je, ni kwa kiasi gani kazi ya Yesu msalabani inahatoa uhakika kwamba madhara fulani ya dhambi na laana hayatashuhudiwa tena na waaminio katika Yesu? Tumemuua KijanaWetu Hiki ndicho kichwa cha kitabu cha wanandoa wapendwa Wakristo ambao, wakikiri kuponywa kwa mtoto wao mwenye kisukari, walimwona akifa kutokana na ukosefu wa insulini, na vivyo hivyo walijiona wakishtakiwa na kupatikana na hatia ya kuzembea katika kifo cha mtoto wao. Je, ungewezaje kuwaelekeza waumini wapya kuomba maombi ya imani kwa ajili ya uponyaji, mabadiliko, na baraka, huku, wakati huo huo, wakimruhusu kutumia Mungu haki yake ya kumzuilia mtoto wake chochote kwa ajili ya nidhamu, mafunzo, na makuzi?
2
3
4
M A S O M O Y A B I B L I A
4
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker