Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

176 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Muktadha wa kihistoria ambao ulimzunguka Yesu wakati wa kutokea kwake katika huduma yake ya hadharani (yaani, utawala wa Warumi juu ya ulimwengu wa wakati huo) uliathiri sana mwitikio wa watu wa wakati wake kwa habari ya aina yake ya Ufalme alioutangaza. Vikundi hatari vilihusisha Masadukayo, Mafarisayo, Waesene, Wazeloti, na Maherodi. Dhana ya Wayahudi ya Ufalme wa Mungu wakati wa Yesu, ililochochewa na ukandamizaji waliokuwa wakiupitia kutoka kwa mamlaka za kisiasa, na ilihusisha imani kwamba Ufalme wa Mungu ungekuja kwa nguvu, kurejesha ulimwengu unaoonekana na kuokoa wanadamu kutoka katika udhibiti wa Shetani. Yesu, kwa upande mwingine, alitangaza Ufalme uliokuwa ndani yake, na alidhihirisha uhalisia wake kupitia maisha yake na kazi zake za uponyaji na kutoa pepo. Kama unapenda kujifunza kwa kina baadhi ya mawazo yaliyomo katika somo hili la Kupingwa kwa Masihi , jaribu kusoma vitabu vifuatavyo: Ladd, George Eldon. Crucial Questions About the Kingdom of God . Grand Rapids: Eerdman’s, 1952. Willis, Wendell, wah. The Kingdom of God in 20th-Century Interpretation . Peabody, MA: Hendrickson Publishers, 1987. Kuelewa asili ya upinzani ambao Masihi aliupata ni msingi wa kuanza kujiandaa kwa huduma ya ufalme leo. Baada ya kutafakari sana juu ya uthibitisho wa kibiblia wa namna Masihi alivyoweza kustahimili upinzani wa mara kwa mara dhidi ya maisha na kazi yake, lazima utumie fundisho hili katika maisha na huduma yako ya Kikristo. Ikiwa unamtumikia Yesu, tayari unajua mengi kuhusu ukweli wa maandiko haya rahisi. Sasa, katika maisha na huduma yako leo, ni kwa jinsi gani Roho Mtakatifu angetaka utiwe moyo katika mapambano yako mwenyewe dhidi ya dhambi, shetani, mwili wako, na ulimwengu? Je, ni mapambano gani ya ndani unayopigana dhidi ya tamaa na shauku, ni ushawishi gani wa nje unaokusudia kukuingiza katika hali na matendo ya kutokutii katikati majaribu ya ulimwengu, na ni migogoro gani isiyo ya kawaida unayopitia dhidi ya uongo na mashaka ya adui? Jaribu kubainisha yale maeneo ambayo Bwana angetaka ufikirie katika maisha yako na huduma ya vitendo, na utafakari katika maombi ni hatua gani angetaka uchukue ili kushiriki tena katika vita kama askari na mtoto wa Kristo.

Marudio ya Tasnifu ya Somo

Nyenzo na Bibliografia

Kuhusianisha Somo na Huduma

4

M A S O M O Y A B I B L I A

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker