Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 4 | USHAHIDI WA AGANO J IPYA KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUPINGWA KWA MASIHI / 177

Ikiwa kuna jambo lililo wazi katika mafundisho ya Maandiko Matakatifu, ni ukweli kwamba vita vingi vya muumini hufanywa katika kundi; adui hapigani nami tu, bali anapigana nasi. Kwa faida ya msaada, uwajibikaji, na ukuaji, unahitaji maombi na ushauri wa wengine wanaohusika katika vita na mapambano sawa na yale unayokabiliana nayo, kama ambavyo nao pia wanakabiliana nayo (1 Pet. 5:8-10). Usisite kuwaomba waamini unaowaamini kukuombea hasa katika maeneo unayohitaji kuimarishwa na msaada wa Mungu. Mungu atasikia na kujibu maombi ya watoto wake wanaoamini (Yak. 5:16). Utafuteni uso wa Bwana pamoja kwa nguvu na uweza wake, wala msife moyo; anajua tuna haja naye na tunahitaji upaji wake (Flp. 4:13).

Ushauri na Maombi Ukurasa wa 100  7

KAZI

Yohana 15:18-20

Kukariri Maandiko

Ili kujiandaa kwa ajili ya kipindi, tafadhali tembelea www.tumi.org/ books ili kupata kazi ya kusoma ya wiki ijayo, au muulize mkufunzi wako.

Kazi ya Usomaji

Wakati huu ni muhimu uwe umeainisha na kuthibitisha mapendekezo yako kuhusu kazi yako ya huduma kwa vitendo, na iwe imepitishwa na mkufunzi wako. Hakikisha kwamba unapanga shughuli zako mapema, ili usichelewe kukabidhi kazi zako.

Kazi Zingine

4

M A S O M O Y A B I B L I A

Katika somo letu linalofuata, Ufalme wa Mungu: Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu , tutaangazia nia ya Mungu ya kuondoa uasi wote na kutokutii kama matokeo ya Anguko – Mungu anakuwa Shujaa katika ulimwengu huu ulioanguka. Yesu wa Nazareti ni uwepo wa Ufalme unaotimizwa, huku utawala wa Mungu ukidhihirishwa katika kuvaa kwake mwili, kifo, ufufuo, na kupaa kwake. Hadithi ya Ufalme ni hadithi ya Yesu, na nia ya Mungu ni kurudisha ulimwengu chini ya utawala wake ndani yake. Tunamsifu Mungu kwa hadithi yake ya ufalme, na shauku yako kama mwanafunzi wa Neno lake Takatifu!

Kuelekea Somo Linalofuata

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker