Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

194 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

r. Mtume Yohana katika maono ya Ufunuo, Ufu. 1:12-20

D. Ufufuo wake unamaanisha nini ?

1. Ufufuo wake ni ishara ya cheo chake cha Uwana mtakatifu, Rum. 1:4.

2. Ufufuo wake ni utimilifu wa agano la Daudi kama Petro anavyosema katika mahubiri yake ya Pentekoste, Mdo. 2:25-31.

3. Ufufuo wake pia unadhihirisha kwamba Kristo sasa ndiye chanzo cha uzima mpya kwa wote wanaomwamini (1 Yoh. 5:11-12).

1

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

4. Ufufuo wake ni njia ya kuadhimishwa kwake katika ukuu na kuinuliwa kama Kichwa cha Kanisa, Efe. 1:20-23.

5. Ufufuo wake unathibitisha kwamba kuhesabiwa haki kwetu mbele za Mungu kumetimizwa kupitia yeye pekee, Rum. 4:25.

6. Na Yesu, kama Bwana wa uzima, alifufuliwa kuwa limbuko la kundi kubwa la waamini watakaoshiriki utukufu wake wa ufufuo, 1 Kor. 15:20-23.

E. Kupaa ni ishara inayoonekana ya mamlaka na ukuu wa Yesu, kuinuliwa kwake kama Shujaa wa ushindi wa Mungu, na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Mungu. Sambamba na kuanzishwa kwa Ufalme wa Mungu kupitia Yesu wa Nazareti, Yesu amepaa mbinguni. Kwa nini?

1. Kama ishara inayoonekana ya mamlaka na ukuu wake, aliyeabudiwa juu na malaika watakatifu wa Mungu, Ebr. 1:3-4

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker