Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 1 | UFALME WA MUNGU : KUZ I ND I L IWA KWA UTAWALA WA MUNGU / 195

2. Kama Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Mungu na Bwana wa mavuno, Mt. 28:18-20

3. Kama Kichwa cha Kanisa, Efe. 1:20-23

4. Kama ishara ya ukuu wake na ubwana kamili juu ya yote, Flp. 2:9-11

Hitimisho • Yesu wa Nazareti ndiye mkuu zaidi, Mtiwa-Mafuta wa Mungu ambaye kupitia yeye ahadi za Ibrahimu zimetimizwa. • Ndani yake, Bwana wa wote, uwepo wa Ufalme ulidhihirika, na kuonyeshwa kupitia kuvaa kwake mwili, kifo, ufufuo, na kupaa kwake. Maswali yafuatayo yamekusudiwa kukusaidia upitie maudhui yanayohusiana na Yesu kuzindua na kutimiza Ufalme wa Mungu. Jibu maswali, ukikazia fikira kwenye “mawazo makuu” na kanuni zinazohusiana na wazo la kuzinduliwa kwa Ufalme, na pia jukumu la Yesu katika kuleta Ufalme katika uhalisia. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko! 1. Ni kwa njia zipi inaweza kusemwa kwamba Yesu wa Nazareti alijitangaza kuwa utimilifu wa ushuhuda wa Agano la Kale kwa habari ya Masihi? 2. Ni zipi baadhi ya ishara katika maisha ya Yesu zinazothibitisha kwamba ndani yake Ufalme umezinduliwa na kutimizwa kwa kadiri fulani? 3. Elezea uhusiano uliomo katika kifungu cha maneno, “Ufalme ambao upo tayari/ambao haujakamilika”. Ni katika njia zipi Ufalme unaweza kusemwa kuwa tayari upo? Ni katika njia zipi tunaweza pia kujua kwamba Ufalme bado uko katika wakati ujao? 4. Nini maana ya neno parousia , na linahusianaje na wazo zima la Ufalme ambao bado unakuja? 5. Je, Yesu analinganishwaje na Mwana-Kondoo wa Pasaka wa sherehe ya Agano la Kale? Ni katika njia zipi Yesu angeweza kusemwa kuwa ni Mwana-Kondoo wa Pasaka wa Agano Jipya?

Ukurasa wa 109  7

1

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu Ukurasa wa 110  8

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker