Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

196 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

6. Kifo cha Kristo kinadhihirisha nguvu za Ufalme wa Mungu uliopo katika njia mbili zipi leo? 7. Kulingana na Paulo, kwa nini ufufuo ni fundisho kuu la Ukristo? Tunajuaje kwamba ufufuo wa Yesu ni hakika – kuna ushahidi gani kwa hilo? 8. Ni baadhi ya mambo gani ambayo ufufuo unamaanisha kuhusu Ufalme? 9. Kama ni ishara ya mamlaka na Ukuu wa Yesu, kupaa kunachangiaje uelewa wetu kwamba katika Yesu, Ufalme umezinduliwa? Somo hili linaangazia njia muhimu ambazo Agano la Kale na Agano Jipya zinashuhudia kwamba Ufalme wa Mungu umezinduliwa, kupitia ahadi ya agano la Mungu kwa Ibrahimu na Mababa, kupitia kabila la Yuda na ukoo wa Daudi, na hatimaye katika Yesu Kristo, ambaye kama Christus Victum (yaani kupitia kifo chake msalabani) na Christus Victor (yaani kupitia ufufuo wake na kupaa kwake) ameuingiza Ufalme wa Mungu katika enzi hii ya sasa. • Mungu alifanya upya ahadi yake ya agano kutoka kwa Abrahamu, kwenda kwa Isaka na Yakobo, kwa watu wa Israeli, kwa kabila la Yuda, kwa ukoo wa Daudi, na hatimaye kupitia Yesu Kristo, ambaye ametimiza Ufalme katika maana ya mwisho kupitia maisha na kazi yake. • Katika Yesu wa Nazareti, ahadi za agano za Ibrahimu na ahadi za kinabii za ushuhuda wa Agano la Kale kwa habari ya Masihi zimetimizwa. Yesu ndiye utimilifu wa ahadi ya Kimasihi. • Katika maisha na huduma ya Yesu, mamlaka na nguvu za utawala wa Mungu zimezinduliwa na kudhihirishwa. Ijapokuwa sehemu kubwa ya utimilifu wa Ufalme huo ni ya wakati ujao, tayari Ufalme huo umedhihirishwa katika umwilisho wa Yesu duniani. • Kifo cha Yesu kilivunja nguvu za shetani na wafuasi wake, na pia kulipa adhabu ya dhambi zetu. Akiwa dhabihu kuu na Kuhani Mkuu, Yesu amelipa yote kwa ajili ya wanadamu, kama Christus Victum . • Ufufuo wa Yesu ulitokea: ishara ya cheo chake cha Uwana wa kiungu, utimilifu wa agano la Daudi, uthibitisho kwamba Mungu ametusamehe dhambi zetu, na ishara ya limbuko ya wale wote ambao siku moja watafufuliwa kuingia katika uzima wa milele kwa njia ya imani katika yeye.

UHUSIANISHAJI

Muhtasari wa Dhana Kuu

1

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker