Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
198 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
MIFANOHALISI
Ugunduzi Uletao Ushindi Ndugu mmoja Mkristo mwaminifu, baada ya kusikia fundisho kwamba Ufalme wa Mungu tayari upo, alilichukulia kumaanisha kwamba nguvu zote za ufalme na baraka zake zinapatikana kwa ajili yetu leo. Mara moja alianza kufundisha katika darasa lake la shule ya Jumapili kwamba Yesu ameleta Ufalme, na kwa hiyo hatupaswi tena kuingiliwa au kupigwa na shetani. Hasa, alianza kuwafundisha vijana kwamba hawakupaswa tena kuwa wagonjwa, au kukosa pesa, au kutenda dhambi, au hata kukata tamaa kihisia. Kama matokeo ya mafundisho yake, migawanyiko ilizuka kati ya vijana na wazazi wao. Wengine walimuunga mkono ndugu huyo, huku wengine wakithibitisha kwamba “katika ulimwengu tutakuwa na dhiki.” Pande zote mbili zimeenda kwenye Biblia na zimekazia Maandiko hayo ambayo yanaunga mkono hoja zao; kwamba tuna ushindi katika Kristo, au, kwamba tunashindana na kupigana katika ulimwengu huu, na mwili, shetani, na mfumo huu mwovu wa majaribu. Pande zote mbili ambazo kwa namna fulani zimefadhaishwa na kuchanganyikiwa kidogo, wanakuuliza uje na kufafanua maana ya “tayari” katika Ufalme ambao upo “tayari / na bado”. Je, ungeusaidiaje ushirika huu unaotaabika kufikia uelewa wa maana halisi ya neno “tayari” na “bado” kuhusiana na Ufalme wa Mungu? Kila Kitu Ni Kwa Baadaye! Katika kushiriki mafundisho ya somo hili na baadhi ya marafiki kanisani, mwanafunzi mhitimu mgeni wa seminari inayojulikana sana anaanza kusema jinsi mtazamo huu ni wa uzushi. Akiwa anaamini sana kwamba maisha na mamlaka yote ya ufalme yameahirishwa hadi enzi zijazo, mwanafunzi aliyehitimu anaanza kuelezea jinsi Israeli walivyopewa ofa ya ufalme lakini wakaikataa, na kumuua Masihi aliyewaalika. Baada ya kukataa aina ya ufalme ambayo Yesu aliwatangazia, anasema sasa tuko katika enzi ya Kanisa ambayo inakuja kati ya wakati wa ofa ya ufalme ambayo Yesu aliitoa, na wakati wa Ujio wa Pili, ambapo Israeli hatimaye itakubali ofa ya ufalme wa Mungu, na Ufalme wa Daudi utawekwa katika siku zijazo. Sasa, hakuna udhihirisho wa Ufalme uliopo, kila kitu kinachohusika na Ufalme ni cha baadaye. Ungemwambia nini mwanafunzi huyu? Je, maoni yake yanaonekana kuwa na usahihi wowote? Tangu Anguko, Mungu ametafuta kukomesha na kupindua athari zake kwa kuleta utawala wake katika ulimwengu huu wa sasa. Alianza kudhihirisha utawala wake kwa uthabiti kwa kuchukua msimamo kama Shujaa juu ya maadui zake. Kupitia ahadi yake ya agano kwa Abrahamu, Mungu aliazimia kuleta Mzao ulimwenguni
1
Ukurasa wa 110 9
1
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
2
Marudio ya Tasnifu ya Somo
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker