Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 1 | UFALME WA MUNGU : KUZ I ND I L IWA KWA UTAWALA WA MUNGU / 199
ambao ungeponda kichwa cha nyoka na kubariki familia zote za dunia. Ahadi ilifanywa upya kwa mababa, katika Israeli, kwa kabila la Yuda na ukoo wa Daudi. Hatimaye, katika Yesu wa Nazareti na kazi zake, utawala wa ufalme wa Mungu umezinduliwa kwa maana ya mwisho katika ulimwengu huu. Kama Christus Victum , alitukomboa kutoka katika nguvu za shetani, dhambi na kifo, na kama Christus Victor , amefufuka kutoka kaburini na kupaa mbinguni kama Bwana wa wote. Ingawa haujatimizwa kikamilifu, Ufalme umekuja katika nafsi ya Yesu Kristo. Ikiwa una nia ya kufuatilia baadhi ya mawazo ya somo hili Mungu kama Shujaa wa Kiungu , unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo: Dawson, John. Taking Our Cities for God . Toleo la 2. Altamonte Springs: Charisma House, 2001. Lind, Millard. Yahweh is a Warrior: The Theology of Warfare in Ancient Israel . Scottsdale: Herald Press, 1980. Uhusiano wa maana za ushindi wa Yesu una umuhimu mkubwa kwa kila nyanja ya huduma yetu. Sasa ni wakati wa kujaribu kukazia theolojia hii ya juu kwa kuhusianisha elimu hii na mazingira halisi ya huduma kwa vitendo, ambayo utaifikiria na kuiombea katika wiki hii yote ijayo. Roho Mtakatifu anakudokeza nini hasa kuhusiana na utawala wa Mungu, na changamoto yake leo? Ni hali gani inakuja akilini unapofikiria kuhusu ukweli wa kuzinduliwa kwa utawala wa Mungu na maisha yako na huduma yako leo? Jipe muda wa kutafakari mbele za Bwana juu ya mambo haya, naye atakufunulia kweli hizi na kukujulisha kile unachopaswa kufanya kutokana na kile anachokufunulia. Aina ifaayo ya maombi kwa kuzingatia mafundisho ya somo hili ni kuabudu, kusifu, na kushukuru. Kuona azimio la Mungu wa Utatu kuja kutusaidia, kupigana na adui zetu, kupindua athari za Anguko, kumtuma Mwanawe ambaye alimkabili shetani na kifo kwa ajili yetu – upendo huu mkuu unapaswa kuzalisha ndani yetu bubujiko kubwa la sifa na shukrani. Mungu hakutuacha katika hali yetu dhaifu, lakini alitoa kilicho bora yake kwa ajili yetu. Tunapaswa kutafuta njia za kuonyesha maana ya kutumia ushindi wa Yesu dhidi ya adui zetu na kumwona Mungu akifanya kazi kupitia imani yetu nyenyekevu. Labda kuna watu katika familia yako au kanisani, kazini au katika mtaa wako ambao tunaweza kuwainua kwa Mungu kwa njia ya Yesu.
Nyenzo na Bibliografia
1
Kuhusianisha Somo na Huduma
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
Ushauri na Maombi Ukurasa wa 110 10
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker