Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

200 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

KAZI

Luka 11:20-23

Kukariri Maandiko

Ili kujiandaa kwa ajili ya darasa, tafadhali tembelea www.tumi.org/ books ili kupata kazi ya kusoma ya wiki ijayo, au muulize Mkufunzi wako.

Kazi za Usomaji

Soma maeneo uliyoagizwa na uandike muhtasari usiozidi aya moja au mbili kwa kila eneo moja. Katika muhtasari huu tafadhali toa uelewa wako bora zaidi wa kile unachofikiri kilikuwa jambo kuu katika kila eneo husika la usomaji. Huhitaji kutoa maelezo mengi; andika tu kile unachoona kuwa jambo kuu linalozungumziwa katika sehemu hiyo ya kitabu. Tafadhali kabidhi muhtasari huo darasani wiki ijayo. (Tafadhali ona “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” kwenye ukurasa wa 16). Katika somo letu linalofuata, Mungu Baba: Mungu katika Utatu – Ukuu wa Mungu , tutaangalia ushahidi wa kibiblia hukusu Utatu, Nafsi tatu za Mungu. Maandiko yanafundisha kwamba kuna Mungu mmoja tu, na bado Mungu huyuhuyu anajidhihirisha kama Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Washiriki wa Utatu wako katika umoja, utofauti na usawa, Mungu mmoja wa kweli, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Hakika, Mungu wetu Baba Mwenyezi ndiye Mungu wa mbinguni mmoja, wa kweli na wa utukufu. Kumjua vizuri zaidi kutatusaidia kumwakilisha kwa heshima tukiwa watumishi wake. Mungu akubariki unapochunguza utajiri usioelezeka wa Maandiko kuhusu Mungu wetu mkuu na mwenye nguvu! Tafadhali tazama nyenzo zifuatazo katika kitabu cha Theolojia katika Picha: Orodha ya A-Z ya Vielelezo, Chati, Michoro na Makala Muhimu za TUMI : • Mpangilio wa Matukio ya Ufalme wa Mungu , ukurasa wa 298 • Yesu wa Nazareti: Uwepo wa Wakati Ujao , ukurasa wa 544 • Kuishi Katika Ufalme Uliopo Tayari, Ambao Bado Haujaja , ukurasa wa 132 • Dhana za Ufalme , ukurasa wa 27 • Hapo Zamani za Kale , ukurasa wa 47

Kazi Zingine

1

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

Kuelekea Somo Linalofuata

KWA UTAFITI ZAIDI

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker