Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

202 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

kuaminika ya kutafuta ukweli. Tamaduni zetu leo hazina subira wala imani katika imani yoyote ambayo kwanza haina uwezo wa kujithibitisha yenyewe kuwa halali kwa kiwango cha vigezo vya yanayoweza kuelezeka na kupimika. Dini ya Mashahidi wa Yehova ni mfano dhahiri. Kila kitu katika Biblia ambacho hakiwezi kueleweka mara moja kinabadilishwa ili kuendana na mfumo wao wa fikra na mantiki. Kwa mfano, kwa kuwa hawawezi kabisa kumwelewa Mungu kama utatu katika umoja, wanakataa fundisho la Maandiko juu ya Utatu ingawa Biblia inaweka wazi uungu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Katika theolojia yao, Yesu anakuwa malaika mkuu Mikaeli na Roho Mtakatifu anakuwa “kani ya utendaji” kama umeme. Ukitaka kutazama kikamilifu dini iliyovuliwa kabisa mambo yote ya siri na ajabu zote utaiona katika mafundisho ya Mashahidi wa Yehova. Bila kujali ni kelele gani akili zetu zitatupigia, neno rahisi la Mitume linapaswa kuwa msimamo na msingi wetu. Tunapaswa kubatiza kwa jina (umoja) la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Wakati wa ubatizo wa Yesu, Roho Mtakatifu alikuja juu yake kama hua, na sauti ya Baba ikatangaza kwamba amependezwa na Bwana wetu (Mt. 3:17). Andiko la 2 Wakorintho linazungumza juu ya neema ya Yesu, upendo wa Mungu na ushirika wa Roho Mtakatifu (2 Kor. 13:14). Washiriki wote wa Utatu wanarejelewa kama Mungu, na wote wanashiriki sifa zile zile za ukuu. Na bado, Biblia inasema kwamba kuna Mungu mmoja tu, na sio watatu . Utatu ni matokeo ya uthibitisho wa Kibiblia, na si wa mantiki yetu wenyewe. Je, yapasa kutushangaza kwamba Mungu wetu ni zaidi ya mawazo yetu, kwamba Mungu katika ile namna alivyo tu hawezi kujulikana au kueleweka? Na tupige magoti mbele za Bwana Muumba wetu, tukisisitiza kwa moyo wa furaha neno la Bwana wetu katika Mathayo 11: Mathayo 11:27 – Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia. Na tuuthibitishe ukweli wa Maandiko na kumpa Mungu wa mbinguni, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu sifa na heshima. Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Ee Mungu, Wewe usiye na kikomo, wa milele na usiyebadilika, mtukufu katika utakatifu, umejaa upendo na huruma, mwingi wa neema na kweli. Matendo yako kila mahali yanakusifu, na utukufu wako umefunuliwa katika Yesu Kristo Mwokozi wetu. Kwa hivyo

2

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker