Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 2 | MUNGU BABA : MUNGU KAT I KA UTATU – UKUU WA MUNGU / 203
tunakusifu, utatu mtukufu na mtakatifu, Mungu mmoj, milele na milele. Amina. ~ Kanisa la Kipresbiteri la Marekani na Kanisa la Kipresbiteri la Cumberland, Kitengo cha Theolojia na Huduma ya Kuabudu. Kitabu cha Ibada ya Pamoja . Louisville, KY.: Westminister/John Knox Press, 1993. uk. 51
Ee Baba, tumaini langu, Ee Mwana, kimbilio langu, Ee Roho Mtakatifu, ulinzi wangu. Utatu mtakatifu, utukufu ni wako.
~ Compline, Eastern Orthodox, St. Joannikios Appleton, George, mhariri. The Oxford Book of Prayer . Oxford/New York: Oxford University Press, 1988. uk. 183
Fanya mazoezi pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu kwa kutamka andiko la kukumbuka ulilopewa katika kipindi kilichopita: Luka 11:20-23.
Mazoezi ya kukariri maandiko
2
Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walikusudia kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).
Kazi za kukusanya
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
KUJENGA DARAJA
Imani Isiyoleta Maana? Mmoja wa washirika wa kanisa lako, Bi. Jackson, alitembelewa na Shahidi wa Yehova juzijuzi, na tangu wakati huo mazungumzo hayo yanamsumbua. Kwa zaidi ya sa moja Bi. Jackson alisikiliza kwa makani mantiki safi, sahihi, na yenye kuvutia ya Mashahidi waliomtembelea nyumbani kwake. Alihisi kulemewa kabisa wageni hawa walipokuwa wakielezea orodha ya makosa ambayo walisema makanisa mengi huamini. Wakiyakataa makosa mengi na kusema kwamba ni uongo na uvumi tu wa kihistoria, Mashahidi hawa walitoa hoja kwa dhati kabisa dhidi ya fundisho kwamba Roho Mtakatifu ni nafsi, fundisho la Utatu, uungu wa Kristo, uwepo wa kuzimu, wokovu kwa neema, na mengine mengi. Akiwa amechanganyikiwa, mshirika huyu akawauliza Mashahidi, “Nyie watu mnaonekana kuwa mna uelewa wa kila kitu; mnaonekana kutoamini chochote msichoweza kukielewa.” “Ni kweli kabisa,” aliitikia kiongozi wa kundi lile la Mashahidi, “ni kwa nini utake imani isiyoleta maana kwako?” Maneno hayo yamebaki katika kumbukumbu ya mshirika wako tangu yalipoongelewa. Unawezaje kujibu swali la Mashahidi: ni lazima kila kitu katika Biblia kilete
1
Ukurasa wa 116 3
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker