Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
204 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
“maana” kwetu kabla ya kuamini ushuhuda wake? Je, hatupaswi kuamini chochote Biblia inachosema, hata kama kinapita ujuzi na mantiki zetu?
Na Mwenye Kustahili Kusifiwa KulikoWote Akisimamia ukweli kwamba Mungu anastahili ibada ya hali ya juu na iliyobora sana, msimamizi wa huduma ya muziki kanisani kwako ameandaa bajeti yenye ongezeko lisilo la kawaida kwa ajili ya vifaa vya muziki na kikundi cha kuabudu. Akiwa ameguswa sana na mfululizo wa mahubiri ya mchungaji kuhusu sifa za Mungu , anasema sasa ametambua kuwa amekuwa akimtolea Mungu dhabihu kilema , huku akizuilia rasilimali bora kabisa na fedha nyingi kwa ajili ya mahitaji na matamanio yake binafsi. Kwa shauku kubwa na nia ya dhati, alitamka kwamba ikiwa Mungu ni mkuu tena asiye na kikomo, basi anastahili kusifiwa sana! “Namna muhimu zaidi,” alidokeza, “tunayoweza kumuonyesha Mungu huyu mkuu kuwa tunampenda ni kumpa kile kilicho bora zaidi, na hiyo inatakiwa ifanyike haraka!” Kama ungekuwa mjumbe katika kikao hiki, ungeshauri nini kuhusiana na ufahamu wa mzimamizi huyu wa huduma ya muziki juu ya ukuu wa Mungu, na kwamba mtazamo huo unapaswa kuathiri mara moja namna tunavyoendesha shughuli, tunavyotumia fedha na tunavyofanya ibada? Mambo Mengi Bila Sababu ! Anaporudi kutoka seminari, Bill anahuzunishwa kwa sababu, tofauti na yeye mwenyewe, inaonekana hakuna hata mtu mmoja katika kanisa lake anayeonekana kujali kuhusu mambo aliyokuwa akijifunza akiwa seminari. Baada ya mihula mingi ya kupambana na mafundisho makuu ya imani, ana shauku ya kutoa majibu yake kwa maswali yao yote ya kimafundisho, lakini watu wanaonekana hawana swali lolote. Kimsingi, wanaona mijadala ya mafundisho na mingine kama hiyo, kama alivyosema shemasi mmoja, “inakera kabisa; ina mambo mengi bila sababu”. Pana uhusiano gani kati ya uhitaji wa kujua na kutetea yale ambayo Biblia inasema kuhusu Mungu na Ufalme wake na imani ya kawaida ya washirika wengi ambao hushikilia tu ukweli kwamba Biblia ni Neno la Mungu? Una ushauri gani kwa Bill?
2
2
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
3
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker