Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 2 | MUNGU BABA : MUNGU KAT I KA UTATU – UKUU WA MUNGU / 205

Mungu katika Utatu: Ukuu wa Mungu Ukuu wa Mungu (Sifa za Asili)

Mch. Dkt. Don L. Davis

MAUDHUI

Neno la Mungu linasisitiza kwa uwazi kwamba kuna Mungu mmoja tu ( Shema , Kum. 6:4), na bado pia linathibitisha uungu wa Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Fundisho la Utatu ni matokeo ya kukubali fundisho la Biblia juu ya umoja wa Mungu , na wakati huohuo, likithibitisha yale linayosema kuhusu asili ya uungu ya nafsi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Lengo letu katika Sehemu hii, Ukuu wa Mungu , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Fundisho la Utatu linarejelea fundisho la Biblia kuhusu utatu wa nafsi ya Mungu. • Maandiko yanasema kwamba Mungu ni mmoja, na kwamba hakuna mwingine ila Yeye aliye Mungu mmoja, na bado yanasisitiza kwamba Mungu huyo mmoja amejidhihirisha kama Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. • Kila mshiriki wa Utatu (Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu) anazo sifa za Mungu na hufanya kazi kama Mungu, anaitwa Mungu, na hutumia mamlaka kama Mungu. • Biblia inathibitisha umoja wa Mungu na wingi wake vile vile (kwamba Uungu Mtakatifu ni zaidi ya nafsi moja), kwa pamoja nafsi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu zinazungumzwa kama nafsi katika Uungu Mtakatifu. • Kanisa limejaribu kutengeneza namna za kuelewa mafunidisho ya Biblia kuhusu Utatu, huku pakiwa na viwango tofauti vya kukubalika kwayo miongoni mwa waamini. • Ni lazima tusisitize asili ya Mungu ya utatu, tukithibitisha kwamba washiriki wa Utatu, ingawa ni Mungu katika nafsi

Muhtasari

2

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

tatu, kimsingi ni umoja, wana utofauti, na usawa, kwa pamoja wakimkamilisha Mungu mmoja wa kweli, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.

I. Bwana Mungu ni Mungu katika Utatu

Muhtasari wa Maudhui ya Video

A. Mantiki na umuhimu wa kibiblia wa Utatu

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker