Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

246 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (iliyo katika kiambatisho), sali sala ifuatayo:

Kanuni ya Imani ya Nikea na Sala

Eh! Baba mwenye neema na mtakatifu, utupe hekima ya kukufahamu, akili ya kukuelewa, bidii ya kukutafuta, subira ya kukungojea, macho ya kukutazama, moyo wa kukutafakari, na maisha ya kukutangaza kwa uweza wa Roho wa Yesu Kristo Bwana wetu. Amina. ~ St. Benedict. FromWilliam Lane, S. J. Praying with the Saints . Dublin, Ireland: Veritas, 1989. uk. 26.

Fanya mazoezi pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu kwa kutamka andiko la kukumbuka ulilopewa katika kipindi kilichopita: Waebrania 2:14-17.

Mazoezi ya Kukariri Maandiko

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walikusudia kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za Kukusanya

KUJENGA DARAJA

Theolojia katika Kitabu cha Picha Chora picha ambayo inamwakilisha Roho Mtakatifu. Ukishamaliza, ujiandae kuelezea mchoro wako kwa wengine.

4

1

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

Ukurasa wa 128  4

Kuishindania Imani Kanisa katika kila kipindi limekuwa likikumbana na “walimu wa uongo” ambao wanayapindisha Maandiko, wakiyatumia kufundisha mafundisho ambayo ni tofauti kabisa na yale ya Yesu na Mitume wake. Mafundisho haya ya uongo (uzushi) yanaonekana “kujizalisha upya,” na kwa sababu hiyo mawazo yaleyale yaliyokosewa yanapata mawakili wapya katika kila kizazi. Wazo moja lisilosahihi kuhusu Roho Mtakatifu ambalo linajitokeza mara kwa mara ni imani kwamba Roho Mtakatifu ni aina fulani ya nguvu ya kiroho (au ufahamu fulani wa kiroho) lakini sio Nafsi ya Kiungu inayoongea na kutenda kama Mungu Aliye Hai. (Katika nyakati zetu, makundi kama Mashahidi wa Jehova na The Unity School of Christianity yanafundisha mtazamo huu wa uongo). Mafundisho ya kikristo maarufu zaidi katika nyakati za sasa yanalenga kuelezea kazi za Roho Mtakatifu; kile ambacho anafanya kwenye maisha ya waamini.

2

Ukurasa wa 129  5

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker