Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 4 | MUNGU ROHO MTAKAT I FU : NAF S I YA ROHO MTAKAT I FU / 247

Unaweza kufikiri sababu yoyote inayoweza kuonyesha kwamba kufundisha Roho Mtakatifu ni nani kuna umuhimu sawa na kufundisha kazi zake?

Watatu Katika Mmoja Tuna maanisha nini tunaposema kwamba Mungu ni Utatu? Ni vielelezo vipi umevisikia vikitumika kujaribu kuelezea Utatu? Kuna vipengele gani vinavyoonyesha uthabiti na udhaifu katika kila kielelezo?

3

Ukurasa wa 129  6

Nafsi ya Roho Mtakatifu Mpaji wa Uhahi

Mch. Terry G. Cornett

MAUDHUI

Katika sehemu hii tutaangalia kwa makini mada kuu inayounganisha kazi nyingi za Roho Mtakatifu ulimwenguni. Tutaona kwamba Roho ndiye atoaye uhai kwa ulimwengu kupitia kazi yake katika uumbaji na upaji. Tutachunguza baadhi ya ishara za kawaida, majina, na vyeo vinavyotumiwa kumwelezea Roho Mtakatifu katika Maandiko na kuchunguza jinsi kila moja ya ishara, majina na vyeo hivyo inavyochangia katika ufahamu wetu juu ya Roho kama Mpaji wa Uhai. Hatimaye, tutahitimisha kwa mjadala wa jinsi huduma ya upaji uzima ya Roho inavyoleta tumaini la siku zijazo. Malengo yetu kwa sehemu hii, Mpaji wa Uzima , nikukuwezesha: • Kuelezea kwanini somo la kitheolojia la Roho Mtakatifu linaitwa Neumatologia . • Kutoa muhtasari wa mtazamo wa Agano la Kale kuhusu Roho wa Mungu. • Kutumia Maandiko kuelezea kazi ya Roho Mtakatifu ya kutoa uzima katika kuumba na kuuhifadhi ulimwengu. • Kutambua ishara kuu zinazohusiana na Roho Mtakatifu katika Maandiko na kuonyesha ni kwa namna gani zinachangia katika uelewa wetu juu ya Roho kama mpaji wa uzima. • Kuelezea ni kwa namna gani majina na vyeo vya Roho Mtakatifu vinatusaidia kumwelewa kama mpaji wa uzima. • Kuelezea kwanini huduma ya Roho ni chanzo cha tumaini.

Muhtasari

4

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker