Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
248 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
I. Mpaji wa Uhahi Tunamwamini Roho Mtakatifu, Bwana na Mpaji wa Uzima, atokaye kwa Baba na kwa Mwana, ambaye pamoja na Baba na Mwana anaabudiwa na kutukuzwa, ambaye alinena na manabii.
Muhtasari wa Maudhui ya Video
II. Pumzi ya Mungu yenye Nguvu
A. Somo kuhusu fundisho la Roho Mtakatifu linajulikana kama Neumatologia (Pneumatology) .
1. Pneuma ni neno la Kiyunani lenye maana ya “upepo au pumzi au roho.”
2. Neno la kiebrania ruach (ambalo linatumika katika Maandiko ya Agano la Kale) linabeba maana ileile ya msingi ya “upepo au pumzi au roho.”
B. Yamkini namna bora ya kumwelezea Roho Mtakatifu kama anavyoelezewa katika Maandiko ya Agano la Kale ingeweza kuwa “Pumzi ya Mungu yenye nguvu.”
4
1. Katika Maandiko ya Kiebrania, Pumzi ya Mungu ni nguvu yenye uwezo ambayo inaharibu (Kut. 15:10; Isa. 11:4) na kuumba (Zab. 33:6).
Ukurasa wa 130 7
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
Neno la Kiebrania linalotafsiriwa kama ‘roho’ ni ruach . Mzizi wa neno r-w-ch , ambako nomino hiyo imechipukia, maana ya kwanza kabisa ni “kupumua kwa nguvu kutumia pua.”... Neno ruach linatafsiriwa kama kupumua kwa nguvu kubwa, kwa vurugu, ambapo hapa ni kinyume cha neno neshamah , ambalo kwa kawaida linamaanisha, kupumua kwa utulivu.... Neno ruach linatumika mara kwa mara kama upepo; kama mara themanini na saba kwa jumla. Katika hizi, thelethini na saba zinaongelea upepo kama wakala wa Yehova, ambapo mara nyingi ni upepo ule unaoharibu, na mara zote ni upepo mkali na wenye nguvu.... ruach-adonai [Roho wa Bwana] ni udhihirisho wa uweza wa Mungu uletao uzima na nguvu katika maisha ya mwanadamu..... ruach-adonai hawezi kuzuiwa
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker