Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
276 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
anasema jambo lile lile, “Nilikuwa tayari kujionesha kwao wasiouliza habari zangu. Nilikuwa tayari kuwapokea wale wasionitafuta” . . . Dhambi ya mwanadamu wa kwanza imenyong’onyesha na kudhoofisha sana hiari yake kiasi ambacho baada ya hapo hakuna mtu anayeweza kumpenda Mungu kama inavyompasa au kumwamini Mungu au kufanya mema kwa ajili ya Mungu, isipokuwa neema ya rehema ya Mwenyezi Mungu imemtangulia.
~ Baraza la Orange (529 B.K)
2. Pili, tunamaanisha kwamba kwa kuwa wokovu huja kwa njia ya imani pekee, hauwezi kupatikana na mtu yeyote kwa jitihada binafsi. Wokovu unaweza kupokelewa kama zawadi ya bure tu, ambayo mtu hawezi kuistahili kupitia matendo ya wema. Wokovu ni zawadi kamili ya neema ya Mungu.
Ukurasa wa 144 8
1
H U D U M A Y A K I K R I S T O
a. Efe. 2:8-9
b. Mdo. 20:24
c. Gal. 2:21
d. Tendo lolote jema au la haki tunalotenda ni matokeo ya neema ya Mungu inayofanya kazi ndani yetu. Matendo mema ni matokeo ya wokovu sio sababu yake. Hakuna tendo lolote jema linalotupatia kibali chochote cha ziada mbele za Mungu. Hakuna yeyote anayeweza kuwa mwema kiasi cha kutosha ili kupata uhusiano kuwa na Mungu au uzima wa milele pamoja naye katika Ufalme wake. Tumemiminiwa neema yake kwa sababu ya Kristo na yale ambayo kazi yake imetutendea. Matendo yetu mema ni mwitikio kwa neema ambayo Mungu ametupa. Tena, Kama vile Mtume Yohana anavyosema, “Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza” 1 Yoh. 4.19.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker