Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 1 | THEOLOJ I A YA KAN I SA : KAN I SA KAT I KA I BADA / 277

II. Ibada ni Mwitikio wa Kanisa kwa Neema ya Mungu. Mara zote ibada ni jukumu pekee na la muhimu zaidi la Kanisa kwa sababu ni mahali pa kuanzia kuishi kwa neema. Katika ibada, tunatambua kama vile Yakobo alivyoandika katika Waraka wake kwamba, “Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga” Yak. 1:17a. A. Matukio mawili muhimu katika ibada ya Kikristo (mlo na kuoga) Katika kila utamaduni wa Kikristo, Meza ya Bwana na ubatizo ni sehemu muhimu za namna tunavyopata uzoefu wa neema ya Mungu itendayo kazi miongoni mwetu. Hata hivyo, Wakristo wanatofautiana kuhusu namna matendo haya ya ibada yanavyoidhihirisha neema ya Mungu katika Kanisa. Baadhi ya makanisa huita Meza ya Bwana na ubatizo kama “sakramenti” na wanayaelewa mambo hayo kama “njia ya neema” wakati wengine huyaita “maagizo” na kuyaelewa kama ushuhuda wa neema ya Mungu. Wacha nieleze tofauti. 1. Sakramenti kwa kawaida hufafanuliwa kama “ishara ya nje na inayoonekana ya neema ya ndani na ya kiroho.” Wale wanaotumia neno sakramenti huona ubatizo na Meza ya Bwana kama njia ambayo kwayo neema ya Mungu hutujilia. 2. Ingawa Wakatoliki na Waothodoksi wana sakramenti nyingi, Waprotestanti kwa kawaida wamehifadhi neno sakramenti kwa ajili ya ubatizo na Meza ya Bwana pekee. Sakramenti hizi mbili zina nafasi ya pekee katika historia ya Kanisa kama “njia muhimu ya neema” kwa sababu zilianzishwa moja kwa moja kwa amri ya Yesu. Wale wanaofafanua Meza ya Bwana na ubatizo kama sakramenti wangesema kwamba vinapopokelewa kwa imani, Mungu kwa neema anafanya kazi ndani yetu ili kutimiza ahadi zake. B. Maana ya “sakramenti”

Ukurasa wa 145  9

1

H U D U M A Y A K I K R I S T O

Ukurasa wa 145  10

Ukurasa wa 146  11

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker