Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 1 | THEOLOJ I A YA KAN I SA : KAN I SA KAT I KA I BADA / 279

c. Mk. 16:15-16

d. 1 Pet. 3:20-22

“Kanuni thelathini na Tisa za Dini” ambazo ni ukiri wa msingi wa makanisa yenye mapokeo ya KiMethodisti na ya KiAnglikana inaelezea fundisho la kisakramenti la Ubatizo kama hivi. “Wale wanaopokea Ubatizo katika namna sahihi wanapandikizwa katika Kanisa; ahadi za ondoleo la dhambi, na kufanywa wana wa Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu zinatiwa sahihi na kutiwa muhuri; Imani inathibitishwa, na Neema inaongezeka kwa nguvu ya maombi kwa Mungu.”

~John H. Leith, ed. Creeds of the Churches. Louisville: John Knox Press, 1983. Uk. 275-76

1

H U D U M A Y A K I K R I S T O

2. Ni muhimu kuelewa kwamba wale wanaotazama ubatizo kama sakramenti hawafundishi habari ya kuzaliwa upya au mara ya pili kwa njia ya ubatizo. Kuzaliwa upya kwa njia ya ubatizo ni imani potofu inayodai kwamba ni ubatizo pekee unaomwokoa mtu kwa sababu tu tendo la ubatizo limefanywa. Nyakati fulani huko nyuma, Kanisa Katoliki lilionekana kufundisha jambo lililokuwa likikaribiana sana na hili, lakini leo mafundisho ya Kikatoliki na Kiprotestanti yanakubali kwamba jambo kuu katika ubatizo ni imani. Baba wa Kanisa Gregori wa Nyssa alisisitiza kwamba ikiwa mtu anabatizwa lakini hakuuambatanisha ubatizo na toba ya kweli basi, “katika hali ya namna hii maji hubaki kuwa maji tu, kwa maana kipawa cha Roho Mtakatifu hakionekani kwa njia yoyote ndani yake yeye ambaye amebatizwa kwa namna hiyo tangu kuzaliwa kwake.”

Ukurasa wa 146  13

B. Wale wanaofafanua ubatizo kama agizo wanautazama kama ishara ambayo mtu hutangaza utambulisho wake katika Kristo na Kanisa lake. Ubatizo ni muhimu kwa mtu kuingizwa katika Kanisa.

1. Msaada wa Maandiko kwa mtazamo wa ubatizo kama agizo au ishara:

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker