Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 1 | THEOLOJ I A YA KAN I SA : KAN I SA KAT I KA I BADA / 281

2. Unaweza pia kusikia ikiitwa ekaristi (ambayo ina maana ya “chakula cha shukrani”), Ushirika, au Meza ya Bwana. Chakula cha Bwana kilitolewa kwa Kanisa na Yesu mwenyewe usiku kabla ya kukamatwa kwake.

Katika Meza ya Bwana kuna mwendelezo wa kufanywa upya

kwa agano kati ya Mungu na Kanisa. Neno ‘ukumbusho’ (anamnesis) linarejelea si tu mtu kumkumbuka Bwana bali pia Mungu kumkumbuka Masihi wake na agano lake, na ahadi yake ya kurejesha Ufalme. Wakati wa mlo huu yote haya huletwa mbele za Mungu katika maombi na maombezi. ~ R. S. Wallace. “Lord’s Supper.” Evangelical Dictionary of Theology. Walter A. Elwell, Mh. Grand Rapids: Baker, 1984. uk. 653.

B. Iliasisiwa na Yesu Kristo

1. Mt. 26:26-29

2. 1 Kor. 11:23-26

1

C. Ilifanywa mara kwa mara tangu siku za kwanza za Kanisa na kuendelea

H U D U M A Y A K I K R I S T O

Ushahidi wote wa awali. . . ulionyesha kwamba ingawa vipengele vya ibada [ya Kanisa la kwanza] havikuwa na mpangilio maalum, tukio kuu la ibada ya kila juma katika Siku ya Bwana lilikuwa ni sakramenti ya Meza ya Bwana.

~ R. G. Rayburn. “Worship in the Church.” Evangelical Dictionary of Theology. Walter A. Elwell, mh. Grand Rapids: Baker, 1996. uk. 1193.

[Meza ya Bwana] ingeweza kuadhimishwa kwa njia inayofaa zaidi, kama ingetolewa kwa Kanisa mara kwa mara, angalau mara moja kwa juma. . . . Inatupasa kila mara kuhakikisha kwamba hakuna mkutano wa Kanisa unaofanywa bila neno, maombi, meza ya Bwana, na [kukusanya pesa kwa ajili ya maskini].

~ John Calvin. Institutes . 4.17.43-44.

Sababu ya pili ya kwa nini kila Mkristo anapaswa [kushiriki ushirika] mara nyingi kadiri awezavyo, ni kwa sababu faida za kufanya hivyo ni kubwa sana. . . . Neema ya Mungu iliyotolewa humo inatuthibitishia msamaha wa dhambi zetu, kwa kutuwezesha kuziacha. Kama miili yetu inavyoimarishwa kwa mkate na divai, ndivyo roho zetu zinavyoimarishwa kwa ishara hizi za mwili na damu ya Kristo. Hiki ndicho chakula cha nafsi zetu: Hutupa nguvu ya kutekeleza wajibu wetu, na hutuongoza kwenye ukamilifu. Kwa hiyo, ikiwa tunajali kwa namna yoyote ile amri iliyo wazi ya Kristo, ikiwa tunataka msamaha

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker