Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
282 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
wa dhambi zetu, ikiwa tunataka nguvu ya kuamini, kumpenda na kumtii Mungu, basi hatupaswi kupuuza fursa yoyote ya kupokea Meza ya Bwana; basi tusiipe kisogo kamwe karamu ambayo Bwana wetu ametuandalia. Hatupaswi kupuuza tukio lolote ambalo majaliwa mema ya Mungu hutupatia kwa kusudi hili. Hii ndiyo kanuni ya kweli: Tunapaswa kuipokea mara nyingi kadiri Mungu anavyotupa nafasi. Basi mtu ye yote asiyeipokea, bali anatoka katika meza takatifu, wakati vitu vyote vimetayarishwa, ni ama haelewi wajibu huu, au hajali amri ya mwisho ya Mwokozi wake kabla ya kufa, msamaha wa dhambi zake, kuimarishwa kwa nafsi yake, na kuburudishwa kwa tumaini la utukufu.
~ John Wesley. “Sermon 101: The Duty of Constant Communion.” The Works of John Wesley . Toleo la 7-8. uk. 148.
1
D. Chakula cha Bwana kinapaswa kuliwa kwa toba na imani.
H U D U M A Y A K I K R I S T O
1. Sababu mojawapo iliyowafanya wanamatengenezo wa Kiprotestanti kuachana na makanisa ya Kikatoliki kwa mara ya kwanza ni kwa sababu walihisi kwamba sakramenti zilikuwa zikitazamwa kama kitendo cha kiganga badala ya neema ya Mungu iliyopokelewa kwa imani.
Ukurasa wa 147 16
2. Meza ya Bwana si kama ibada ya kichawi ambayo hupelekea kutolewa kwa neema kwa kule kushiriki tu katika tendo hilo.
Wanamatengenezo wa awali wa Kiprotestanti walipinga fundisho la Kikatoliki ambalo lilijulikana kama ex opere operato . (Hiki ni kifungu cha maneno ya Kilatini kinachomaanisha “kwa msingi wa tendo lililotendwa.”) Hili lilimaanisha kwamba sakramenti iliyotolewa ilileta matokeo yaliyotarajiwa pasipo kujali kama mtu anayeitoa au yule anayeipokea alikuwa akitenda kwa imani. Wanamatengenezo walilipinga hilo na kudai kwamba lilikuwa limefanya watu wazione sakramenti kama uganga au uchawi: kwamba kubatizwa au kula Mlo wa Bwana kulifanya mtu awe Mkristo. Jibu lao lilikuwa kwamba mtu anakuwa Mkristo na kukua kama Mkristo “kwa imani pekee.” Wakatoliki wanaendelea kufundisha ex opere operato isipokuwa wamebadili fundisho lao ili kukazia upya kwamba kupokea sakramenti kwa imani si wazo la Kiprotestanti tu bali ni jambo
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker