Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 1 | THEOLOJ I A YA KAN I SA : KAN I SA KAT I KA I BADA / 283
la lazima kwa maoni ya Kikatoliki vilevile kwa kusema kwamba “[sakramenti] hutangulia imani” na kwamba, “zikiadhimishwa ipasavyo katika imani, sakramenti hutoa neema.”
~ Catechism of the Catholic Church . Liguori, MO: Liguori Publications, 1994. uk. 291-293.
E. Kuna mitazamo minne muhimu ya Kikristo juu ya Meza ya Bwana (Tazama Meza ya Bwana: Mitazamo Minne kwenye ukurasa wa ….. [page #]???? katika Theolojia katika Picha: Orodha ya A-Z ya Vielelezo, Chati, Michoro na Makala Muhimu za TUMI :).
1. Ubadilishaji ni imani kwamba mkate na divai hugeuka mwili na damu halisi ya Yesu Kristo. Huu ni mtazamo wa Meza ya Bwana unaoshikiliwa na Wakristo wa Kikatoliki.
Ukurasa wa 147 17
1
a. Mt. 26:26
H U D U M A Y A K I K R I S T O
b. Yn. 6:53-60
Kwa muujiza wa mikate na samaki na kutembea juu ya maji, siku iliyotangulia, Kristo hakuwaandaa tu wasikilizaji wake kwa ajili ya hotuba tukufu [ya Yohana 6] yenye ahadi ya Ekaristi, lakini pia aliwathibitishia kwamba yeye kama Mwenyezi Mungu na mtu, alikuwa na uwezo ulio juu na usio zuiwa na kanuni za asili, na kwa sababu hiyo, angeweza kutoa chakula hicho kisicho cha kawaida, si kingine, zaidi ya Mwili na Damu yake mwenyewe. ~ Joseph Pohle. “Eucharist.” Readings in Christian Theology . Vol. 3. Millard Erickson, mh. Grand Rapids: Baker, 1973.
2. Muungano ni imani kwamba mkate na divai vinakuwa mwili na damu halisi ya Yesu bila kukoma kuwa mkate na divai. Huu ndio mtazamo wa Meza ya Bwana unaoshikiliwa na makanisa ya Kilutheri. Mtazamo huu unakubali wazo la msingi lililojadiliwa hapo juu kwamba mwili halisi na damu ya Yesu viko katika mkate na
Ukurasa wa 148 18
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker