Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
284 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
divai lakini una maelezo tofauti ya jinsi vinavyokuwepo pamoja.
3. Mtazamo wa tatu ni mtazamo wa Matengenezo . Makanisa ya Presbiteri na ya Reformed hufundisha kwamba mwili na damu ya Kristo hutolewa kwetu katika Karamu, sio kimwili, lakini kiroho kupitia nguvu na uwepo wa Roho Mtakatifu. Mapokeo haya yanaonyesha kwamba katika kifungu cha Yohana 6 ambacho Yesu anafundisha kuhusu kula mwili wake, anaendelea kusisitiza jambo hili kama kweli ya kiroho: Yn. 6:60-63 – Basi watu wengi miongoni mwa wanafunzi wake waliposikia, walisema,, Neno hili ni gumu, ni nani awezaye kulisikia? 61 Naye Yesu akafahamu nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanalinung’unikia neno hilo, akawaambia, Je! Neno hili linawakwaza? 62 Itakuwaje basi, mmwonapo Mwana wa Adamu akipaa huko alikokuwako kwanza? 63 Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima. Yesu yuko katika sakramenti hii ila si kimwili bali kiroho. . . . Watu wake wanampokea sio kwa mdomo bali kwa imani; hawapokei mwili na damu yake kama vitu vya kimwili, bali mwili wake uliovunjwa na damu yake iliyomwaga. Kwa jinsi hiyo unganiko linaashiriwa . . . ni unganiko la kiroho na la ajabu kwa sababu ya kujiliwa na Roho Mtakatifu. Ubora wa sakramenti hii kama njia ya neema haupo katika ishara wala ibada, wala mhudumu, au neno, lakini upo katika matokeo ya kutembelewa na Roho Mtakatifu.
1
H U D U M A Y A K I K R I S T O
~ Charles Hodge. Systematic Theology . Abridged edition. Grand Rapids: Baker, 1992. uk. 496-498.
a. Kol. 3:1
b. Yn. 16:7
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker