Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 1 | THEOLOJ I A YA KAN I SA : KAN I SA KAT I KA I BADA / 285

Ingawa mapokeo mengi ya Kipentekoste ni ya kiUkumbusho, mwanazuoni wa Kipentekoste Gordon Fee anatetea maoni sawa na ya Calvin anaposema: “Kwa kweli, mtu atakuwa hajakosea sana kuuona uwepo wa Roho Mtakatifu katika Meza ya Bwana kama namna ya Paulo ya kuuelewa uwepo halisi. Mfano wa Israeli kula ‘chakula cha Roho,’ na ‘kinywaji cha Roho’ katika 1 Wakorintho 10:3-4 walau unaliruhusu wazo hilo.”

~ Gordon Fee. Paul, the Spirit and the People of God. Peabody, MA: Hendrickson Publishers, 1996. uk. 154.

4. Mtazamo wa kiUkumbusho unaamini kwamba mkate na divai ni ishara tu ya mwili na damu ya Kristo na hutusaidia kukumbuka yale aliyotufanyia.

1

a. Tofauti na mitazamo mitatu ya kwanza ambayo huitazama meza ya Bwana kama sakramenti, Mtazamo wa kiUkumbusho huitazama meza ya Bwana kama agizo.

H U D U M A Y A K I K R I S T O

Meza ya Bwana haina nguvu ya kumzaa mtu upya/mara ya pili, haina neema ya utakaso. Hakuna kitu cha kichawi au cha ajabu kuhusu asili yake. Ni ishara ya uhusiano wa mwamini na Kristo, ambaye peke yake hufanya utakaso. Ishara za nje zilizobuniwa na Kristo mwenyewe ni ishara za nguvu ya upatanisho na upendo wa msamaha wa dhabihu yake kuu, ambayo ilileta mtokeo mara moja na kwa zote.

~ Williams Stevens. “The Lord’s Supper.” Readings in Christian Theology. Millard Erickson, mh. Grand Rapids: Baker, 1973.

b. Lk. 22:19

c. 1 Kor. 11:23-24

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker