Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
286 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
F. Kile kinachofanana katika mitazamo hii inayotofautiana kuhusu Meza ya Bwana:
1. Kila sehemu ya theolojia ya Kikristo inaamini kwamba Meza ya Bwana ni:
a. Sehemu muhimu ya ibada ya Kikristo.
b. Amri ya moja kwa moja ya Kristo kwa Kanisa lake.
c. Wasaa unaotusogeza karibu zaidi na Mungu na waamini wenzetu.
1
H U D U M A Y A K I K R I S T O
d. Wasaa unaoturuhusu kushika neema ya Mungu na kumwitikia kwa shukrani na sifa.
e. Ilikusudiwa kupokelewa kwa imani na kutusaidia kuweka imani zetu kamili katika kazi ya Kristo.
f. Wasaa ambao dhambi zinaweza kushughulikiwa na kuwekwa chini ya rehema ya Mungu yenye kusamehe.
2. Tunaweza kutokubaliana juu ya namna Meza ya Bwana inavyosababisha mambo haya kutokea lakini kutoelewana huko kusitufanye tusahau umuhimu wa msingi wa Mlo huu katika maisha yetu ya ibada. Ni zawadi ya neema ya Mungu kwa Kanisa lake.
Hitimisho • Kuabudu ni mwitikio wa Kanisa kwa neema ya Mungu. • Wokovu huja kwa neema ya Mungu na hakuna mwanadamu anayeweza kusema kwamba amejipatia wokovu wake kwa yale aliyoyafanya. • Ubatizo na Meza ya Bwana ni sehemu muhimu sana za ibada ya Kikristo.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker