Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 1 | THEOLOJ I A YA KAN I SA : KAN I SA KAT I KA I BADA / 287

• Kanisa linatofautiana kwenye namna ya kuielewa Meza ya Bwana na ubatizo. Wengine wanaamini kwamba ni sakramenti, yaani, njia ambayo neema ya Mungu inatujia huku wengine wakiamini kwamba ni maagizo ambayo yanaashiria na kushuhudia neema ya Mungu.

Tafadhali chukua muda mwingi kadiri uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yameletwa na video. Maswali haya yaliundwa ili kukusaidia kupitia maudhui ya somo hili kuhusiana na neema ya Mungu kama msingi wa ibada ya Kanisa. Unapojibu maswali haya, jaribu kuunda uthibitisho wa wazi juu ya kile ambacho Maandiko yanafundisha kuhusu neema ya Mungu. Kwa kuwa Wakristo wanaoamini Biblia hutofautiana kuhusu namna neema ya Mungu inavyotujia katika Meza ya Bwana na ubatizo, tafadhali wasikilize kwa karibu na kwa heshima wale ambao wanaweza kutokubaliana nawe darasani. Jibu kwa uwazi na kifupi, na inapobidi tetea jibu lako kwa Maandiko! 1. Sola Gratia inamaanisha nini na kwa nini ni muhimu? 2. Uzushi wa Pelagiani ni nini? 3. Kuna tofauti gani kati ya mapokeo ya Kikristo yanayoelezea ubatizo na Meza ya Bwana kama sakramenti na yale yanayozichukulia kama maagizo ? 4. Je, kuna hoja zipi kuu za kibiblia zinazokubaliana na zinazotofautiana na suala la kuona ubatizo kama “njia ya neema”? 5. Je, kuna maoni gani makuu manne kuhusu Meza ya Bwana? 6. Kwa nini imani kwamba kubatizwa husababisha wokovu ni fundisho lisilo la kimaandiko? Je, hili linatofautianaje na mtazamo wa kisakramenti wa ubatizo? 7. Kwa nini wanamatengenezo Waprotestanti hawakukubaliana na fundisho la Kikatoliki la ex opere operato ? 8. Je, imani ina nafasi gani katika uzoefu wetu wa sakramenti/ maagizo?

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu Ukurasa wa 148  19

1

H U D U M A Y A K I K R I S T O

UHUSIANISHAJI

Somo hili linaangazia njia ya msingi ambayo sisi kama washirika wa Kanisa tunayo katika kumkaribia Mungu, yaani, ule msingi wa neema pekee kwa njia ya imani katika Kristo, na jinsi uzoefu wa neema hii unavyojidhihirisha katika sifa, kuabudu, shukrani

Muhtasari wa Dhana Muhimu Ukurasa wa 149  20

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker