Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

288 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

na ibada ya kweli kwa Mungu kupitia Yesu Kristo. Katika maana moja, kuelewa dhana hizi za msingi ni kiini cha maana halisi ya kulitumikia Kanisa kama mmoja wa viongozi wake, na hutusaidia kung’amua wakati kusanyiko lina afya au linaumwa, kulingana na uzoefu wake wa kibali na neema ya bure ya Mungu katika Kristo, na udhihirisho hai wa shukrani yake kupitia njia yake ya maisha katika ibada. Zifuatazo ni baadhi ya dhana za msingi zinazohusiana na ibada, wito wa kweli wa Kanisa. • Wokovu ni zawadi ya bure kabisa ya Mungu inayopaswa kupokelewa kwa imani na haiwezi kupatikana kwa jitihada au kwa kustahili. • Wanadamu wamefanywa watumwa wa dhambi kiasi kwamba hawawezi kutamani mambo yaliyo sahihi isipokuwa neema ya Mungu ifanye kazi ndani yao kwanza. • Mara zote Mungu ndiye wa kwanza katika kuchukua hatua ya kumleta mtu katika wokovu. “Sisi tunampenda kwa sababu yeye alitupenda sisi kwanza.” • Kwa sababu Kanisa ni jumuiya ya watu ambao wanauzoefu wa neema ya Mungu, ibada ni wajibu na furaha ya Kanisa. • “Mlo na kuoga” (Meza ya Bwana na ubatizo) ni sehemu ya namna ambayo tunashiriki na kukumbuka neema ya Mungu. Hivi ni vipengele muhimu vya ibada ya Kikristo. • Sakramenti ni njia ambayo kwayo neema ya Mungu inatolewa kwetu wakati agizo ni tendo linalokubali neema kupitia utii na ukumbusho. Aina zote mbili za theolojia zinasisitiza kwamba kushiriki katika Meza ya Bwana na ubatizo kuna faida ikiwa tu kutaambatanishwa na toba na imani. • Viongozi wa Kikristo wanapaswa kusoma Maandiko na kuamua kama ni sahihi kuielewa Meza ya Bwana na ubatizo kama sakramenti au kama maagizo. Sasa ni wakati wa wewe kujadili na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu Kanisa katika Ibada. Kuelewa nafasi ya kimkakati ya neema katika kuanzisha uhusiano kati ya Mungu na kusanyiko la waabudu, pamoja na uhuru na wajibu wa kumwinua Mungu ambao Kanisa linao, ni msingi wa kuwa kiongozi wa Mungu leo. Inaweza kusemwa kwamba ni hadi mtu aelewe na aweze kueleza ukweli huu kwa maneno na matendo, ndiyo ataweza kutekeleza uongozi bora katika Kanisa. Pitia maswali haya ili kuona kama unaelewa kikamilifu kweli hizi na maana za maudhui haya, na jinsi ukweli huu unavyohusiana na wewe na mahusiano yako katika huduma. Je, una maswali gani hasa katika mwangaza wa maudhui ambayo umejifunza hivi punde kuhusu ufahamu wako mwenyewe wa kweli hizi? Pengine baadhi ya

1

H U D U M A Y A K I K R I S T O

Kutendea Kazi Somo na Matokeo kwa Mwanafunzi Ukurasa wa 149  21

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker