Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 1 | THEOLOJ I A YA KAN I SA : KAN I SA KAT I KA I BADA / 289

maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi. • Ingawa watu wengi hawajawahi kusikia kuhusu “uzushi wa Pelagiani,” kuna watu wengi wanaoufanya. Ni kwa namna gani mtu ambaye hakuuelewa wokovu kwa njia hii angezungumzia maana ya kuwa Mkristo? • Je, kanisa lako (au dhehebu) linaelewa Meza ya Bwana na ubatizo kuwa ni sakramenti au maagizo? Kwa nini? • Ni mara ngapi kanisa linapaswa kushiriki Meza ya Bwana pamoja? Kwa nini? • Je, ni kwa kiwango gani timu yako ya kuabudu katika kanisa lako inafahamu kikamilifu ukweli na matokeo yanayohusiana na ibada kama wito wa Kanisa? • Pana kiwango gani cha uhuru katika kuabudu katika kanisa lako kwa maana ya mateno ya kimwili na kisaikolojia yanayosisitizwa katika Biblia? Je, maagizo haya ya kupiga kelele, kupiga makofi, na kucheza “vielelezo vya kitamaduni” yapo kwa kiasi gani ukulinganisha na maagizo ya kibiblia ya ibada? Elezea jibu lako. • “Liturujia” ya kanisa lako ikoje, kwa maneno mengine, ni kwa namna gani kanisa lako linapanga ibada na sherehe zake ili “kusimulia Hadithi Kuu” katika ibada zake? Ni nini kinazuia hili kuwa na ufanisi zaidi katika kanisa lako? • Mtu anabadilishaje hali ya kitamaduni ya kutaniko kutoka kuwa na ibada isiyoruhusu mabadiliko, iliyozoeleka hadi kuwa sifa yenye nguvu na yenye uhai? Je, ni hatua gani zinahitajika ili kufikia hali kama hiyo? Kujionyesha Bila Ulazima Kanisa la mahali pamoja lenye idadi kubwa ya wanamuziki na waimbaji wenye vipawa, sasa limeanza kukua kupitia huduma ya kuabudu yenye nguvu na ubora wa hali ya juu. Hata hivyo, baadhi ya watu wameanza kulalamika kwa sababu kiongozi wa muziki amefanya iwe ngumu zaidi kwa wale wanaoitwa “waabudu wa kawaida” kuwa kwenye timu ya kuabudu au bendi ya sifa. Waimbaji wote lazima wafanyiwe majaribio kwa ajili ya kupima ubora wa sauti zao na uwezo wao wa kusoma muziki, na hakuna wanamuziki wanaoruhusiwa kujiunga kwenye bendi ya sifa kama hawawezi kusoma muziki na kuufuata mpangilio mzuri (lakini mgumu) wa muziki kwa nyimbo zilizochaguliwa. Kiongozi wa muziki ana msimamo imara kwamba Mungu ni mkuu na kwa sababu hiyo ibada

1

H U D U M A Y A K I K R I S T O

MIFANOHALISI

1

Ukurasa wa 149  22

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker