Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
290 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
yetu inapaswa kuwa bora zaidi kadiri iwezekanavyo. Je, ungekuwa na ushauri gani kwa kiongozi wa huduma ya muziki endapo angekuomba utoe maoni kuhusu uelekeo wa ibada katika kanisa hili?
Huwezi Kunifanya Niabudu Kiongozi mpya wa ibada kanisani amekuwa akisisitiza haja ya madhihirisho ya vitendo, ya nje au ya kimwili wakati wa ibada. Ana nguvu sana katika maoni yake kwamba tunapaswa kutumia njia mbalimbali ambazo Maandiko yanazungumza katika kuonyesha upendo wetu kwa Mungu – kupiga makofi, kuinua na kupunga mikono yetu, kupiga kelele, kucheza, kupiga magoti, kunyamaza, kulala kifudifudi, kupiga kelele za furaha – tunapaswa kuonyesha upendo wetu kwa Mungu kwa miili yetu. Kundi dogo lakini lenye msimamo kanisani linapingana vikali na jambo hili, na linataka kukomesha msisitizo huu kuhusu madhihirisho haya ya nje. Kwa sababu kimsingi, huu sio mchezo wa mpira wa miguu, bali ni ibada kwa Mwenyezi Mungu. Mabishano yanazuka miongoni mwa washirika kuhusu kile ambacho kinafaa zaidi kwa kanisa hili. Je, ungewasaidiaje kutatua suala hili? Neema Pekee Mchungaji anamshuhudia binti mmoja kuhusu Yesu na kumwalika kuhudhuria kanisani. Binti huyo anajibu, “Kwa sasa siko vizuri sana kufanya hivyo. Kiukweli ninavutiwa sana na dini na mambo mengine lakini ninataka kuweka maisha yangu sawa kwanza. Nikishaweka sawa baadhi ya vitu, basi nitakuja kanisani.” Mchungaji anapaswa kumwambia nini binti huyu? Kushuka kwa ajili ya Bwana Bendi mpya ya kusifu yenye maadhi ya jazi, fanki na roki inayojiita Selah imeibuka kanisani. Wameazimia kuipeleka sifa na kuabudu kwenye kiwango kipya kabisa cha nguvu katika kusanyiko, lakini wanafanya hivyo kwa aina ya sauti inayoendana na wimbo wa “ in your face ” wakiambatanisha na aina fulani ya onyesho ambalo lina wafuasi wengi hapo kanisani, kiasi kwamba hata baadhi ya watenda kazi wa kanisa, wanavutiwa nalo. Kundi hili la Selah linajipatia umaarufu mkubwa katika matamasha yao ya Jumamosi jioni, na limekuwa likitumiwa sana na Bwana katika baadhi ya huduma za uinjilisti hapo mjini. Hata hivyo, unapowasikiliza, wanaimba kama bendi za kidunia. Kiuhalisia, nyimbo zao nyingi hutumia mdundo wa nyimbo maarufu za muziki wa pop zilizowekewa tu maneno ya Kikristo. Baadhi ya watu wamekiri kwamba huwa wanaenda kwenye matamasha yao kwa ajili ya kucheza tu! Ungewashaurije Selah
2
1
H U D U M A Y A K I K R I S T O
3
4
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker