Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
292 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
na sasa ni fursa kwako kufanya mazoezi ya ujuzi huu, hasa kwa kuuhusianisha na maisha yako mwenyewe. Tafakari juu ya kweli hizi na uone ni ukweli upi au kweli zipi ambazo unaweza kuhitaji kuzitafakari na kuziombea katika wiki hii yote ijayo. Uwe tayari kwa namna Roho Mtakatifu anavyoweza kukutaka usisitize kweli hizi unapowahudumia wale walio chini ya uangalizi wako wiki hii, na umwombe hekima unapotumia kweli hizi katika mazingira yako. Omba kwa Mungu kwa ajili yako mwenyewe na wale unaowahudumia, ili upate kuelewa hasa na kufahamu nguvu ya neema ya Mungu inayobadilisha maishani mwako na kwenye maisha ya wale unaowafundisha. Mwombe Roho Mtakatifu aufanye upendo wa Kristo kuwa halisi zaidi katika maisha yako binafsi, na utafute uwezo wake kwa namna unavyoweza kuwa huru zaidi katika kuelezea sifa na shukrani zako kwa Mungu kwa jinsi alivyo na kwa yale aliyoyafanya maishani mwako. Zaidi sana mwombe Bwana ufahamu katika mambo hayo, maeneo, tabia, au mazoea yanayoweza kukuzuia kutoa sifa zaidi na bora kwa Mungu katika maisha yako, kulingana na wito wetu wa kuleta furaha na heshima ya juu kwa Mungu.
Ushauri na Maombi Ukurasa wa 150 23
1
H U D U M A Y A K I K R I S T O
KAZI
Waebrania 10:19-22
Kukariri Maandiko
Ili kujiandaa kwa ajili ya darasa, tafadhali tembelea www.tumi.org/ books ili kujua kazi ya kusoma ya juma lijalo, au muulize Mshauri wako.
Kazi ya Usomaji
Soma maeneo uliyoagizwa na uandike muhtasari usiozidi aya moja au mbili kwa kila eneo moja. Katika muhtasari huu tafadhali toa uelewa wako bora zaidi wa kile unachofikiri kilikuwa jambo kuu katika kila eneo husika la usomaji. Huhitaji kutoa maelezo mengi; andika tu kile unachoona kuwa jambo kuu linalozungumziwa katika sehemu hiyo ya kitabu. Tafadhali kabidhi muhtasari huo darasani wiki ijayo. (Tafadhali ona “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” kwenye ukurasa wa 16).
Kazi Zingine
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker