Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

296 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

taswira zenye thamani sana ni ile ya mchungaji. Alijiita “Mchungaji Mwema,” yule ambaye, kwa kutii amri ya Baba yake, angetoa uhai wake kwa furaha kwa ajili ya kondoo, ushirika wake uliokombolewa. Katika kila nyanja ya maisha na huduma yake Bwana wetu anasimama kama mtoa huduma kwa wale ambao walikuwa na uhitaji, bila kujali makundi, hali, au nafasi. Iwe ni kukaa katika mazungumzo na mmoja wa watawala katika Israeli (Nikodemo) au kufanya urafiki na mwanamke Msamaria mpweke, aliyedharauliwa, Bwana wetu alitoa ushahidi wa wazi wa moyo wake wa kujali, moyo wenye asili ya uchungaji wa kweli. Bwana wetu hakuwa na ubaguzi wala upendeleo, na kamwe hakuonekana kuwakemea au kuwadharau watu ambao alikutana nao na kuwahudumia. Alikutana na kila mtu kwa wakati kusudiwa na katika hatua kusudiwa ya mahitaji yake maalum. Katika mifano yote wakilishi ya huduma yake katika Agano Jipya, Bwana wetu aliheshimu utu na thamani ya kila mmoja, iwe, mtoto, mwanamke, au mwanamume. Bwana wetu hakuamini kwamba “kipimo kimoja kinawafaa wote” katika suala la kuwajali watu aliokutana nao katika huduma yake. Badala yake, alikuwa mwangalifu kuheshimu hali binafsi na upekee wa hali ya kila mtu, na kuufanya mwitikio wake ufae katika hitaji, upungufu na mzigo husika wa mtu husika. Aina hii ya kujali ambayo ni maalum na yenye kuifaa hali husika, ndio moyo na roho ya huduma ya kichungaji, na pia ndio sababu ya kwanini pana utekelezaji mdogo wa sanaa ya uchungaji leo hii. Wakati ambapo wachungaji wengi wanaona nafasi ya mchungaji kiongozi ni kama ya Mkurugenzi Mtendaji wa kidini ambaye “hachafui mikono yake” kwa kujihusisha na taarifa mbalimbali za maisha ya watu, tunahitaji sana aina mpya (au tuseme, ya zamani kweli) ya uongozi wa kichungaji. Kuna haja kubwa ya kutazama upya asili ya huduma ya kibiblia, aina ya huduma ambayo inalenga katika kukidhi mahitaji ya watu binafsi, familia fulani, mitaa na jumuiya maalum. Hebu tazama tena kujali kwa ajabu kwa Bwana wetu kwa watu maalum – mjane wa Naini, Batimayo kipofu, Zakayo mtoza ushuru, na mwenye pepo wa Wagerasi. Katika kila tukio ni Bwana yule yule mwenye upendo, anayejali, anayefariji, lakini pia katika kila tukio neema na utunzaji wake hutolewa kwa namna fulani. Bwana wetu hakuwa wa kuonyesha upendo akiwa mbali, hata kwa urefu wa mkono tu. Alikaribia kiasi cha kutosha kuwagusa wale aliowahudumia, na kama matokeo ya upendo wake maalum na wa pekee kwa kila kondoo katika muktadha wa maisha yao, alibadilisha maisha yao. Je, ni vihamasishi na vichocheo vya aina gani vitakavyotuwezesha kupata watu walio tayari kutoa aina hii ya huduma yenye kuchosha, na yenye gharama kubwa kwa wale wanaohitaji sana uchungaji wa kiroho? Waefeso 4 inadokeza kwamba ni Mungu pekee ndiye hutoa wachungaji, watu wenye vipawa na wanaopatikana kwa ajili ya watu wake, watu hawa ni kama Bwana wetu, wako tayari

2

H U D U M A Y A K I K R I S T O

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker