Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 2 | MI S I NG I YA UONGOZ I WA K I KR I S TO : K I ONGOZ I WA K I KR I S TO KAMA MCHUNGA J I / 297
kutoa uhai wao kwa ajili ya kondoo. Ni Mungu pekee anayeweza kutoa aina ya uongozi wa Kikristo ambao watu wake wanahitaji, walezi ambao watafuata mfano wa Bwana wetu na kuwa aina ya wachungaji wanaojitoa dhabihu kama yeye alivyokuwa, dhabihu ambayo ilifikia kilele kwa tendo lake la ajabu la kufa kwa niaba yetu. Kwa kuzingatia uhaba wa wachungaji wanaomcha Mungu kwenye miji yetu, tunahitaji kumwomba Mungu kwa bidii na pasipo kukoma atupe kile alichowaahidi watu wake wa Israeli karne nyingi zilizopita: “nami nitawapa ninyi wachungaji wanipendezao moyo wangu, watakaowalisha kwa maarifa na fahamu” (Yer. 3.15). Tunahitaji sana wachungaji ambao, kama Bwana wetu mpendwa, watayatoa maisha yao kwa ajili ya kondoo. R. Robert Cueni ametoa muhtasari wa kuchekesha, mzuri, na wa kweli wa safari ya kutoa huduma kama mchungaji: Kuwa mchungaji ni . . . • Kutumia miaka mitatu kusoma theolojia ya utaratibu na kugundua kwamba maoni ya kisomi zaidi ambayo watu huyaitikia ni “Mungu anakupenda.” • Kutokuwa na pesa za kutosha kulipa bili zako na kuwa na wakati mwingi wa kuhesabu baraka zako. • Kupokea barua mbili za watu wasiojulikana katika wiki moja – moja ikirekebisha sarufi katika mahubiri ya Jumapili iliyopita na nyingine ikiwa na pesa za kupewa familia iliyo na matatizo. • Kuishi karibu na ndugu mara chache lakini kuishi karibu na marafiki kila wakati. • Kujitahidi usicheke unapoombwa kusema neno la baraka katika kuwekwa wakfu kwa mtambo mpya wa kusafisha maji taka katika mjini wako. • Kutumia mara zote hata muda wa ziada katika kazi lakini mara chache kuhisi hitaji la kutazama saa. • Kuungana na watoto wa Mungu katika hatua zote za mabadiliko ya maisha. • Kushiriki furaha ya harusi, kuzaliwa kwa mtoto, ubatizo wa mwamini, na machozi katika hospitali na katika nyumba ya matanga. • Kulazimisha tumaini kwa wale ambao wamefika mwisho. Mungu na atupe sisi sote, kwamba anatuita kwenye uchungaji au la, kuwa watunzaji kama Bwana wetu, na tuwe tayari kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya ndugu zetu, kwa utukufu wa Mungu kwa njia ya Kristo.
2
H U D U M A Y A K I K R I S T O
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker