Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
298 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
Baada ya kukariri na/au kuimba Ukiri wa Nikea (uliopo katika Nyongeza), sali sala ifuatayo Maombi kwa ajili ya wachungaji. . .
Kanuni ya Imani ya Nikea na Sala
Ee Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, uliyemtuma Mwanao sio kutumikiwa bali kutumika, na uliyemfanya kuwa kichwa Kikuu cha Kanisa, umtenge na kumweka wakfu mtumishi wako huyu kwa ajili ya kazi ya huduma. Mpe hekima yako, na katika shauri atende kwa hekima kama mtu aliye na nia ya Kristo. Mpe roho yako ya huruma kwa ajili ya mahitaji ya watu na umjaze na upendo ili aweze kujali kwa upole kila nafsi ambayo kwa neema yako unaipenda. Uimarishe na kustawisha imani yake kwako na katika tunu za Kanisa lako, ili ainue imani ya Wakristo wenzake. Fanya kujifunza kwake kuwe na maana na kazi yake katika Kanisa lako izae matunda. Na utupe neema sisi sote tunaofanya kazi pamoja, tukitafuta kujua mapenzi yako, tuweze kuendeleza kazi yako mahali hapa na duniani kote; kwa utukufu wake yeye aliyewahubiria wafungwa habari njema, Kristo Bwana wetu. Amina.
~ John E. Skoglund. A Manual of Worship. Valley Forge, PA: Judson Press, 1968. uk. 256.
2
H U D U M A Y A K I K R I S T O
Pitia upya na mwenzako, andika na/au jikumbushe kifungu cha mstari wa kumbukumbu uliopewa wakati wa kipindi cha darasa kilichopita: Waebrania 10:19-22.
Mapitio ya Kukariri Maandiko
Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yani hoja kuu ambazo waandishi walitaka kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).
Kazi za Kukusanya
KUJENGA DARAJA
Mchungaji Asiye wa Kichungaji Imekuwa mtindo wa kawaida sasa kwamba wachungaji viongozi wengi wa makanisa makubwa hukabidhi jukumu la uchungaji kwa “watenda kazi” wanaofanya kwa namna ya kawaida sana kazi ya kuwashauri walioshuka moyo na waliofiwa, kuwatembelea wagonjwa, na kuwahudumia watu binafsi na familia ambazo kimsingi ndio sehemu kubwa ya kanisa. Jukumu la mchungaji kiongozi ni kuwa mtu wa “mbele”, “sura ya kanisa mbele ya umma”, yule anayefundisha katika nyakati muhimu za huduma ya hadhara ya kusanyiko, iwe kwenye televisheni, redio, au mtandao. Aina hii ya
1
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker