Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 2 | MI S I NG I YA UONGOZ I WA K I KR I S TO : K I ONGOZ I WA K I KR I S TO KAMA MCHUNGA J I / 299

matukio imeunda ukweli wa “Mchungaji asiye wa kichungaji,” mtu anayeitwa “mchungaji” wa kanisa, lakini kwa kweli, hafanyi huduma ya kichungaji kwa familia halisi za kanisa au kwa watu binafsi. Una maoni gani kuhusu aina hizi za mienendo katika kanisa? Je, asili ya wito wa kichungaji ni kwa ajili ya kuwahudumia watu binafsi na familia maalum au unaweza kuchunga kusanyiko la washirika 3,000 au 5,000 au hata 10,000? Je, ni halali kukabidhi karibu majukumu yote ya kichungaji kwa wengine, huku bado ukiwa na nafasi ya “mchungaji”? Ndugu X kwenye Televisheni Ni Mchungaji Wangu Sambamba na hilo, watu wengi sasa hivi huhusianisha mamlaka yao ya kiroho na ule uangalizi wa kichungaji unaotolewa na watangazaji katika matangazo mbalimbali ya kidini kwenye televisheni au redio. Si jambo la ajabu leo hii kukutana na waamini wanaodai kwamba namna walivyo na hata mamlaka yao ya kiroho yanatoka kwa huyu, yule, au mhubiri mwingine wa televisheni. Wananunua mafundisho yao, “kuhudhuria na kufuatilia” maonyesho yao kwenye redio na televisheni, na hujiambatanisha na mikazo yao, mitazamo, na mipango yao. Wanatoa kwenye huduma zao, na kushirikiana na wafuasi wenzao. Je, inawezekana au inafaa kudai kwamba mtu anayefundisha kwenye redio, televisheni, au kwenye mtandao ndio mamlaka yako ya kiroho, na kumuona kama mchungaji wako ? kinakaribia kupotea. Hapa tunawazungumzia wale wachungaji waaminifu ambao wamejitoa bila ubinafsi kwa ajili makusanyiko madogo, yasiyojulikana ambayo yalihitaji mwongozo mwaminifu wa mtumishi aliyekomaa kiroho, ambaye alikuwa tayari kumimina maisha yake kwa ajili ya wale walio wadogo katika Kristo jijini humo. Wengi wa wachungaji hawa wapendwa hawakupata mafunzo rasmi ya kitheolojia, lakini walitumikia makusanyiko madogo ya mijini kwa malipo kidogo au bila malipo yoyote, na kwa kawaida iliwalazimu kufanya Kazi zingine ili kuchunga makundi yao. Hata hivyo, licha ya magumu na kujidhabihu, watumishi hao waliyatoa maisha yao kwa ajili ya wengine. Kinachovutia kutambua ni kwamba wengi wa wachungaji hawa waliohudumu kwa njia hii walilelewa na kukuzwa katika jukumu hili, yaani, walijifunza sanaa hii kutoka kwa wengine ambao walikuwa wametoa aina hii ya huduma kwa maskini. Inazidi kuwa nadra kupata wale walio tayari kujitoa kwa kiwango hiki cha kutokuwa na ubinafsi na kujidhabihu, hasa kwa ajili ya kusanyiko ambalo linaweza kutoa msaada mdogo wa kifedha. Je, tunawezaje kurejesha “sanaa hii iliyopotea” ya kuwaandaa Sanaa Iliyopotea Kizazi kizima cha wachungaji wa mijini ambao walilelewa na kukuzwa katika sanaa ya kutoa huduma kwa maskini na walioonewa

2

2

H U D U M A Y A K I K R I S T O

3

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker