Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

300 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

wachungaji ambao bila ubinafsi watajali kusanyiko ambalo halitaweza kumudu kuwalipa mishahara, faida, na marupurupu yanayojulikana katika makanisa makubwa zaidi?

Kiongozi wa Kikristo kama Mchungaji ( Poimenes ) Vielelezo, Mafunzo, na Utekelezaji

Mch. Dk. Don L. Davis

MAUDHUI

Neno la Mungu linatoa vielelezo vitatu vya wazi na mifano ya kile nachofanya mchungaji kama mlezi kwa watu wa Mungu ambao ni kundi lake. Mchungaji ni mlezi ambaye huhakikisha kwamba watu wa Mungu wanapokea lishe, malisho, matunzo na huduma inayofaa. Zaidi ya hayo, mchungaji ni mlinzi na msimamizi mwenye jukumu la kuwalinda watu wa Mungu dhidi ya wanyama waharibifu au hali zozote ambazo zingetaka kuwadhuru au kuwaangamiza. Hatimaye, mchungaji ni kiongozi aliyeitwa kwenda mbele ya watu wa Mungu na kuwaongoza katika utimilifu wa mapenzi ya Mungu kwa maisha yao binafsi na ya kusanyiko. Zaidi ya hapo awali, kanisa la mjini linahitaji wachungaji ambao watalisha, kulinda, na kuwaongoza wanafunzi wa Kristo waliopo mijini katika kukomaa katika Kristo na kutoa ushuhuda kwa Ufalme wa Mungu katika miji. Mungu anatoa ahadi zisizo na shaka kwa wale wanaotimiza kwa uaminifu kazi yao ya kuchunga kundi la Mungu – watapokea taji ya utukufu isiyofifia Mchungaji Mkuu atakapotokea wakati wa Ujio wa Pili. Lengo letu katika somo hili, Kiongozi wa Kikristo kama Mchungaji : Vielelezo, Mafunzo, na Utekelezaji , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Neno la Mungu linatoa vielelezo vitatu vya wazi na mifano ya kile anachofanya mchungaji kama mlezi kwa watu wa Mungu ambao ni kundi lake: mchungaji kama mlezi, mlinzi na kiongozi. • Mchungaji ni mlezi ambaye huhakikisha kwamba watu wa Mungu wanapokea lishe, malisho, matunzo na huduma inayofaa. • Pamoja na hayo, mchungaji ni mlinzi na msimamizi mwenye jukumu la kuwalinda watu wa Mungu dhidi ya wanyama waharibifu au hali zozote ambazo zingetaka kuwadhuru au kuwaangamiza. • Mwisho kabisa, mchungaji ni kiongozi aliyeitwa kwenda mbele ya watu wa Mungu na kuwaongoza katika utimilifu wa mapenzi ya Mungu kwa maisha yao binafsi na ya kusanyiko.

Muhtasari

2

H U D U M A Y A K I K R I S T O

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker