Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 2 | MI S I NG I YA UONGOZ I WA K I KR I S TO : K I ONGOZ I WA K I KR I S TO KAMA MCHUNGA J I / 301

• Kwa sababu ya matatizo na changamoto za kipekee za jumuiya za mijini, zaidi ya hapo awali, kanisa la mjini linahitaji wachungaji ambao watalisha, kulinda, na kuwaongoza wanafunzi wa Kristo waliopo mijini katika kukomaa katika Kristo na kutoa ushuhuda kwa Ufalme wa Mungu katika miji. • Mungu anatoa ahadi zisizo na shaka kwa wale wanaotimiza kwa uaminifu kazi yao ya kuchunga kundi la Mungu – watapokea taji ya utukufu isiyofifia Mchungaji Mkuu atakapotokea wakati wa Ujio wa Pili.

I. Vielelezo na Mifano ya Uchungaji

Muhtasari wa Maudhui ya Video

A. Mchungaji ni mlezi. Mchungaji ni mlezi, anayehakikisha kwamba kundi la Mungu linapata lishe na malisho sahihi, matunzo na huduma.

2

1. Kama Mchungaji wa Israeli, jukumu la kipekee la Mungu lilikuwa kuwapatia watu wake chakula na lishe ambayo ingewafanya wakue, waimarishwe, na wafaidishwe na utele wa uongozi wake.

H U D U M A Y A K I K R I S T O

a. Isa. 40:11

Mtume anaagiza kwamba watu kama hao wawe walimu. Awe mtawala mvumilivu. Ajue wakati anaoweza kulegeza hatamu. Mwanzoni na aogopeshe, na kisha apake asali. Na awe wa kwanza kutekeleza yale anayofundisha. ~ Commodianus (c. 240, W), 4.214., DavidW. Bercot, mh. A Dictionary of Early Christian Beliefs .

b. Yer. 23:4

c. Eze. 34:23

2. Mchungaji ni mlezi; huwezi kuchunga kama huna kundi.

3. Mchungaji hatachunga kundi ikiwa hana moyo kwa ajili ya kundi hilo, Yer. 3:15.

Peabody, MA: Hendrickson, 1998. uk. 159.

4. Mchungaji ni mlezi si mtu wa kukandamiza au mwenye kutishia, 1 Pet. 5:3.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker