Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 1 | TAFAKAR I FUP I YA K I THEOLOJ I A / 37
Hitimisho Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini imejikita katika theolojia rahisi na ya vitendo inayojumuisha kufanya upya fikra zetu kuhusu watu wanaoishi katika umaskini, kupima mawazo yetu ya awali juu ya umaskini dhidi ya mada kuu za Biblia, na kuthibitisha ukweli wa msingi kuhusiana na kufanya kazi ya kupambana na umaskini. Maswali yafuatayo yalikusudiwa kukusaidia kutafakari juu ya maudhui ya kitabu cha Kanisa Lisilo la Kawaida , Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini , na video “ Tafakari Fupi ya Kitheolojia ”. Jibu kwa uhakika na kwa ufupi (tafakari maswali haya na uyajibu katika Jukwaa na uwe tayari kuyajadili katika mkutano wetu wa ana kwa ana). 1. Je, unaamini kukosa ufahamu wa kibiblia kuhusu maskini ni tatizo ambalo linaweza kutatuliwa? Muhimu zaidi, unaamini kwa uthabiti kuwa ni tatizo linalostahili kutatuliwa? 2. Watu wengi hujisikia vibaya inapotokea mada ya umaskini, hasa ikiwa hawajawahi kuupitia. Zaidi ya maadili ya kazi ya kiprotestanti yaliyotajwa, unafikiri kwa nini hili linawapa shida? 3. Tofauti na kuwa kipaumbele cha ufalme, kuna sababu zipi tatu kuu za kufanya kazi ya kupambana na umaskini katika misingi ya kibiblia? Je, kuna sababu halali za kutoizingatia? Je, una mpango gani wa kurekebisha na kusawazisha mitazamo hii ili kusonga mbele? 4. Jinsi unavyotumia muda wako, talanta, na hazina yako kwa ajili ya wale walio katika umaskini inaonyesha kwamba una shauku ya kumpenda jirani yako. Toa ushahidi wa vitendo wa kile unachofanya sasa katika maisha yako kuhusu hili. 5. Je, unadhani ni jambo gani muhimu zaidi unaloweza kufanya ili kutumia mambo ambayo umejifunza katika maisha yako? Somo hili linatoa theolojia ya vitendo kwa ajili ya utendaji katika kazi ya kiukombozi dhidi ya umaskini. • Mara nyingi sana tunaruhusu mawazo yetu ya kijamii kufunika mawazo ya kibiblia kwa habari ya wale walio katika umaskini. • Wengi wa wahusika wa Biblia walikuwa watu ambao waliishi katika umaskini na kufanya kazi ndani ya mazingira hayo.
Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu Ukurasa wa 28 6
1
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
UHUSIANISHAJI
Muhtasari wa Dhana Kuu
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker