Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

38 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

• Agano la Kale linasisitiza kanuni ya kutengeneza njia za fursa kwa faida ya watu maskini. • Yesu hakuwa tajiri alipoishi duniani na alifanya huduma hasa miongoni mwa watu wa kawaida. • Yesu alionyesha kujali kwa namna ya kipekee kwa habari ya watu maskini. • Yesu alionya dhidi ya utajiri na kukemea ukosefu wa haki za kiuchumi.

Sasa ni wakati wa wewe kujadili na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu somo letu, Tafakari Fupi ya Kitheolojia . Je, una maswali gani, ukizingatia mambo ambayo umejifunza hivi punde?

Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake Kwa Mwanafunzi

1

MFANOHALISI

K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I

Baada ya kukamilisha somo hili, rejea mfano halisi ulioelezwa hapo awali katika somo hili. Je, unaweza kutoa jibu gani la tofauti, kwa kuzingatia maudhui ya somo hili? Mtumishi kijana wa mjini ambaye anasimamia mafunzo ya watu wanaojitolea kwa ajili ya programu ya kufundisha masomo ya ziada kwa niaba ya shule mojawapo katika mtaa maskini amekuja kwako kutafuta ushauri. Kazi yake ni kutoa semina elekezi kabla ya watenda kazi hao wa kujitolea kupewa watoto wa kufanya nao kazi. Amegundua kuwa mara kwa mara anaingia kwenye shida. Katika kila semina elekezi mjadala unazuka miongoni mwa watenda kazi wapya wa kujitolea kuhusu sababu za umaskini. Kundi moja linasema kwamba watu ni maskini kwa sababu walifanya maamuzi mabaya katika maisha yao. Wengine wanadai kuwa watu ni maskini kwa sababu ya ukosefu wa haki za kiuchumi. Ni nadra sana kuona kundi lolote likinukuu Maandiko ili kujenga hoja zao. Utampa ushauri gani? Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini imejikita katika theolojia rahisi na ya vitendo inayojumuisha kufanya upya fikra zetu kuhusu watu wanaoishi katika umaskini, kupima mawazo yetu ya awali juu ya umaskini dhidi ya mada kuu za Biblia, na kuthibitisha ukweli wa msingi kuhusiana na kufanya kazi ya kupambana na umaskini.

Ukurasa wa 29  7

Marudio ya Tasnifu ya Somo

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker